Na Jotxe Kasiki,Dodoma CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeendelea kuonesha mchango wake katika kukuza sekta ya ufugaji nyuki...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Airtel Tanzania imeendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa kimkakati na wateja kupitia mashindano ya Airtel Business Monthly Mug Tournament yaliyofanyika katika Klabu ya Gymkhana jijini Arusha, Tanzania. Mashindano hayo yaliwaleta pamoja viongozi wa biashara, wateja, na wadau mbalimbali, yakitoa fursa ya kujenga mahusiano yenye tija, kubadilishana mawazo, na kutambua fursa mpya za ukuaji wa biashara nje ya mazingira ya kawaida ya kikazi sambamba na kutambua na kuunga mkono mchezo wa Gofu nchini. Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Airtel Business, Joseph Vipond, amesema Airtel inaamini ushirikiano imara hujengwa kupitia mawasiliano ya karibu na ushiriki endelevu, huku michezo ikitoa jukwaa bora la kuimarisha mahusiano hayo. Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano kwa Umma wa Airtel Tanzania, Sarah Nassor, amesema mashindano hayo yanaonyesha dhamira ya kampuni ya kujenga uhusiano wa kudumu na wadau kwa kuwashirikisha katika masuala yanayochochea mawasiliano, uaminifu, na ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Moja wa watumiaji wa huduma za Airtel ,Hiten Nathwani, ameipongeza kampuni ya Airtel kwa kuendelea kuboresha huduma zake sambamba na kuwasihi wachezaji Gofu hao kutumia huduma za Airtel.  Kupitia Airtel Business Monthly Mug Tournament, Airtel Tanzania inaendelea kuonyesha kuwa ushirikiano wenye tija hujengwa zaidi ya mahusiano ya biashara kwa kuunganisha watu toka sehemu mbalimbali na kuunganisha jamii ili kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi jumuishi wa kidijitali nchini.
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Kampuni ya GF Vehicle Assemblers imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Hamza S. Johari, amekitaka Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kuwa wabunifu na...
Na. Mwandishi Wetu – Dar es Salaam KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya...
Na Mwandishi Wetu, Dodoma MFUMO wa Supervisory Control and Data Acquisition (SCADA) yameimarisha udhibiti wa upotevu wa mafuta wakati wa...
Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma VIJANA wa Program ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) kutoka Samia Ndogowe AMCOS kutoka Wilaya ya Chamwino...
Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma CHUO Kikuu Mzumbe kimetekeleza jumla ya miradi 27 ya maendeleo yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 15.66...
Na Penina Malundo,Timesmajira Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50 pamoja na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Infra for Africa...
Na Joyce Kasiki,Dodoma MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anayesomea Sayansi ya Chakula na Teknolojia, Fredrick Joseph,...
