July 3, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ronaldo aomba radhi Mashabiki wa Manchester United

Na Iddy Lugendo, TimesMajira Online

Mshambuliaji wa Manchester United na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichokifanya jana baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Eveton uliyochezwa katika uwanja wa Goodison Park na United walikubali kichapo cha cha bao 1-0.

Kupitia kwenye mtandao wake wa Instagram Ronaldo ametumia ukurasa huo kuomba radhi kwa mashabiki wote wa Manchester United kwa kitendo cha kuvunja simu ya mshabiki kwasababu alikuwa anampiga picha staa huyo akiwa anatoka nje ya uwanja baada ya mchezo dhidi ya Everton kumalizika.

“Si rahisi kamwe kushughulika na hisia katika nyakati ngumu kama vile tunazokabiliana nazo. Hata hivyo, daima tunapaswa kuwa na heshima, subira na kuweka mfano kwa vijana wote wanaopenda mchezo huo mzuri. Ningependa kuomba radhi kwa hasira yangu na, ikiwezekana, ningependa kumwalika mshabiki huyo kutazama mchezo ujao Old Trafford kama ishara ya mchezo wa haki na uanamichezo”.ameandika Cristiano Ronaldo

Baada ya mchezo wa jana Manchester United wanashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza wakiwa na pointi 51, bado wakiwa na matumaini ya kufuzu kushiriki UEFA msimu jao ikiwa ni tofauti ya pointi 6 na Tottenham Hotspur anayeshika nafasi ya nne,huku vinara wa ligi hiyo ni Manchester City pointi 73 wakifuatiwa na livepoor pointi 72 ni tofauti ya pointi moja na leo wanakutana majira ya 18:30 mshindi wa mchezo huo atakuwa nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la msimu huu.