April 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Banda afichua siri chafu za simba dhidi ya Orlando Pirates

Na mwandishi wetu, Timesmajira Online

Mchezaji wa zamani wa klabu ya simba na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Abdi Banda mwenye umri wa miaka 26, amewatahadharisha wanasoka wa timu ya Orlando Pirates kutoka nchini Afrika kusini kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wekundu wa Msimbazi kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho Afrika (CAF).

Vigogo hao Afrika Kusini, Orlando Pirates wameonywa nini watarajie watakapomenyana na Simba SC ya Tanzania katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika katika mchezo wao wa kwanza aprili 17 utakaopigwa uwanja a Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam na mechi ya marudiano aprili 24 huko Johannesburg.

Kabla ya mechi hizo mbili, mchezaji wa zamani wa Simba na Tanzania, Abdi Banda ambaye kwa sasa anakipiga Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Bara (NBC), amewatahadharisha Pirates kuwa makini na mbinu za Simba wanapocheza nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalipa waamuzi ili kupendelea matokeo upande wao.

“Orlando Pirates wakija Dar es Salaam, lazima watarajie mabaya zaidi na wajue kwamba vita itakuwa nje ya uwanja kwa sababu Simba inaungwa mkono na wanasiasa,” Banda alisema akinukuliwa na KickOff.

“Simba itampa mwamuzi fedha, huwa wanatumia mbinu chafu inapocheza nyumbani, lakini ni wazi hawana aina ya ubora ambao Pirates hivyo watajiwekea bajeti ya kushinda nyumbani kwa tofauti kubwa.”

“Ninachojua ni kwamba Pirates itafuzu. nusu fainali baada ya michezo miwili. Ingekuwa hatari kama Pirates wangecheza Johannesburg kwanza,”Banda aliendelea. “Pirates lazima wamtumie Senzo Mazingiza kwa safari ya Tanzania kwa sababu anaijua Tanzania vizuri na aliwahi kuwa Simba hapo awali na sasa yuko Yanga, Yanga watakuwa na furaha kuwasaidia Pirates kwa lolote wanalohitaji kwa sababu ni maadui wa Simba.”

Banda pia amewataka Pirates kubuni mbinu za kukabiliana na mchezaji “hatari zaidi” wa Simba Bernard Morrison, ambaye pia aliichezea Orlando Pirates mwaka 2016 – 2018 Ligi Kuu ya Soka Afrika Kusini.
‘Morrison atataka kulipiza kisasi dhidi ya Pirates’

“Morrison ni mtu ambaye atakuwa tayari kuthibitisha uhakika kwa Pirates kwa kuzingatia kile kilichotokea siku za nyuma. Nafikiri Morrison alikuwa na kutoelewana na Pirates hapo awali kwa hivyo najua
atakuwa nje kuwaonyesha anachoweza kufanya,” aliongeza Banda. “Ana aina hiyo ya mawazo ya kutaka kujithibitisha kwa wale wanaomtilia shaka.

“Tishio lingine kwa Simba ni Pape Ousmane Sakho vinginevyo hawana timu nzuri kama walivyokuwa msimu uliopita, na inaonyesha katika pengo kati yao na Yanga walio kileleni mwa msimamo. Simba imefuzu hatua ya nane bora baada ya kushika nafasi ya pili Kundi D ikiwa na pointi 10 za mechi sita huku Pirates ikimaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi 13 kutokana na mechi sita.