April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika akizungumza na vyombo vya habari katika Makao Makuu ya chama hicho.

Kumekucha CHADEMA

Yapuliza kipyenga kwa wanaotaka kuwania urais kupitia chama hicho kuanza kuchukua fomu, yavikaribisha vyama vinavyotaka kushirikiana katika uchaguzi

Na Penina Malundo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimefungua milango kwa watia nia wa nafasi ya urais wa Chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 kuanza kuchukua fomu za kuomba kusimamishwa na chama hicho kuwania kiti nafasi hiyo.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika akionesha sehemu ya katiba ya chama hicho ambacho ni mwongozo kwa nafasi ya Urais kipengele 1(g) kinacho tangaza kwamba taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hiyo, zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi

Mchakato huo umefunguliwa rasmi jana Juni 3 na ukomo wake itakuwa ni Juni 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema Chama hicho kimetangaza rasmi kuanza kwa mchakato huo kwa lengo la kuwapa nafasi wanachama wake wenye nia ya kugombea urais kujiorodhesha mapema.

Amesema zoezi hilo ni mchakato wa ndani wa Chama hicho ambao kwa sasa wameanza zoezi hilo kisha kufuatiwa na hatua nyingine ambazo zitatangazwa.

“Ikumbukwe kuwa zoezi hili la kufunguliwa kwa milango la watia nia ya urais ni mchakato wa ndani ya Chama ambao upo kikatiba, kanuni, maadili, itifaki, miongozo na taratibu,”amesema Mnyika na kuongeza

“Chama kina muongozo wa kutangaza kusudio la kuwania nafasi za uongozi kwenye vyombo vya uwakilishi serikalini katika muongozo huu umetaja utaratibu wa kutangaza nia ya kugombea na katika muongozo huo kipengele cha 1 (g) cha Muongozo kinatamka kwamba kwa nafasi ya urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa katibu mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa hatua zinazofuata,”amesema Mnyika.

Aidha amesema kwa mamlaka na kanuni hiyo baada ya maamuzi ya vikao vya Chama ,wameona vema kutangaza kuanza kwa mchakato huo. Mnyika amesema kupitia kifungu hicho cha muongozo baada ya taarifa ya watia nia kujadiliwa na Kamati Kuu taarifa zitapitiwa na kutolewa uamuzi kwa hatua nyingine zitakazofuatwa.

“Taratibu nyingine tutatangaza ikiwemo ratiba za uchaguzi yenye kuhusisha tarehe ya uchukuaji fomu, tarehe ya mwisho wa kurudishwa fomu, taratibu za wagombea urais, vikao vya uchaguzi na taratibu nyingine,”amesema Mnyima.

Pia CHADEMA ilisema imefungua milango kwa vyama vingine ambavyo vinania ya kushirikiana na Chama hicho katika kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani kujitokeza. amesema