April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JNIA yasisitiza umuhimu wa wananchi kufatilia taarifa za hali ya hewa

Na Mwandishi wetu, timesmajira

Kituo Cha Hali ya Hewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kimeadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa maendeleo, huku wakiitaka jamii kufatilia taarifa za hali ya hewa ili kuepukana madhara yanayoweza kujitokeza kutokana mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianch

Akizungumza leo Machi 23, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa elimu kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na Shule ya Msingi Bariadi walipotembelea Kituo Kituo Cha Hali ya Hewa JNIA, Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Usafiri wa Anga na Msimamizi wa Kituo Kituo Cha Hali ya Hewa JNIA, Mamala ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) John Mayunga amesisitiza umuhimu wa jamii kufatilia taarifa za haki ya Hewa.

Mayunga amesema kuwa serikali imewekeza nguvu kubwa katika miundombinu ya hali ya hewa ikiwemo kununua vifaa ikiwemo rada pamoja na vifaa vingine vya kupimia hali ya hewa ili kuleta ufanisi wenye tija kwa Taifa.

“Mamlaka ya Hali ya Hewa ina wataalamu wengi waliosoma ndani na nje ya nchi ambao wanafanya kazi kwa uweledi kwa ajili kuisaidia jamii kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo ” amesema Mayunga.

Amesema kuwa TMA inakitengo ambacho kinahusika katika usafiri wa anga kwa kutoa huduma kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa anga unakuwa Salaam muda wote.

Bw. Mayunga amesema kuwa wanaendelea kutoa huduma za taarifa za hali ya hewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kabla ya ndege kuruka, ikiwa angani na wakati wa kutua.

Amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa uweledi katika kuhakikisha waatoa taarifa kwa usahihi.

Ameeleza kuwa mwaka huu kumekuwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo mvua kubwa ambapo maeneo mengi yamepata mafuriko pamoja na ongezeko la joto la juu, hivyo ni muhimu kuwa na utamaduni wa kufatilia taarifa hizo.

“Sisi tunaendelea kutoa tahadhari kwa wakati na siku ya leo tunaadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani kwa kutoa elimu kwa jamii na kujua namna tunavyofanya kazi” amesema Mayunga.

Nao baadhi ya wanafunzi Peter Mazuri kutoka Chuo Kikuu UDSM pamoja na Merry Kigoda wa Shule ya Msingi Bariadi wameishukuru TMA kwa kuwaelimisha kuhusu utendaji wa kazi zao jambo ambalo ni rafiki katika kuhakikisha wanakuwa na uwelewa katika matumizi ya taarifa ya hali ya hewa pamoja na kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

Maadhimisho ya Hali ya Hewa Duniani 2024 yamebeba kauli mbiu isemayo “Kuwa mstari wa mbele kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi”