Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Coca-Cola Tanzania, imezindua kampeni ya kitaifa ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 inayolenga kuwaunganisha mashabiki wa soka nchini,
Kampeni hiyo, kupitia burudani, promosheni mbalimbali na shughuli za kidijitali zitakazowapa fursa ya kushiriki kwa karibu zaidi shamrashamra za michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.
Kampeni hiyo, iliyoanza Juni 11 hadi Julai 19, 2026, inatarajiwa kuwafikia maelfu ya mashabiki wa soka nchini kupitia shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika maeneo ya biashara, kumbi za burudani na majukwaa mbalimbali.
Aidha, kupitia kampeni hiyo, Coca-Cola inalenga kuhamasisha ushiriki wa mashabiki kupitia michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wake wa takribani miongo mitano na FIFA, Coca-Cola inaendelea kutumia nguvu ya soka kuwaleta watu pamoja kupitia hisia, ushindani na furaha vinavyofanya Kombe la Dunia kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo duniani.

Pia, kampeni hiyo itashirikisha zaidi ya maduka 15,000 ya rejareja, migahawa, kumbi za burudani na vituo vya vyakula nchini kote.
Ushiriki wa maeneo hayo unatarajiwa kutoa fursa kwa mashabiki kukutana, kufuatilia mechi na kusherehekea pamoja, huku ukichangia kuongeza shughuli za kibiashara katika kipindi cha mashindano.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Bonite Bottlers, Raman Narayanan alisema soka lina nafasi ya kipekee katika kuunganisha watu kupitia uzoefu na hisia za pamoja.
“Soka ni zaidi ya mchezo; ni nguvu inayowaunganisha watu na jamii kupitia hisia za pamoja.
*Kupitia kampeni hii, tunalenga kuwapa mashabiki wa Tanzania fursa ya kushiriki kikamilifu msisimko wa Kombe la Dunia la FIFA 2026â„¢ na kusherehekea pamoja kila hatua ya mashindano hayo,” alisema.
Kwa mujibu wa Coca-Cola, kampeni hiyo itahusisha burudani mbalimbali, promosheni maalum katika maeneo ya mauzo pamoja na kampeni za kidijitali zitakazowapa mashabiki nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na michuano hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bonite Bottlers, Christopher Loiruk alisema kampeni hiyo imejengwa katika kutambua hisia zote zinazofanya soka kuwa mchezo unaopendwa na mamilioni ya watu duniani.

“Kombe la Dunia huleta hisia mbalimbali kwa mashabiki, kuanzia furaha ya ushindi hadi majonzi ya matokeo yasiyotarajiwa.
“Kupitia kampeni hii, tunataka kuwa sehemu ya uzoefu huo kwa kuwapa mashabiki fursa ya kusherehekea pamoja na kufurahia kila hatua ya mashindano,” alisema.
Wateja pia, watapata fursa ya kushinda zawadi mbalimbali kupitia ununuzi wa bidhaa za Coca-Cola, ikiwemo bidhaa maalum zenye nembo ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 na mikoba ya kumbukumbu iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya mashindano hayo.
Kupitia kampeni hiyo, Coca-Cola inaendelea kuimarisha dhamira yake ya kuunganisha mashabiki kupitia mchezo wa soka,.
Pia, ikiwapa Watanzania fursa ya kuwa sehemu ya shamrashamra za Kombe la Dunia la FIFA 2026 na kusherehekea pamoja moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo duniani.

More Stories
Washindi ‘Kila muamala bao la ushindi’ wakabidhiwa zawadi
Timu 20 kushiriki Mwijage Cup
Wateja Kampeni ‘Kila muamala bao la ushindi’ vicheko