July 28, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania zaidi ya 90 wanufaika ‘ ikiingia tu goli’

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online

KAMPUNI ya huduma za fedha kidijitali Mixx imewataka Watanzania kuendelea kutumia huduma zake huku ikitangaza kuwa droo ya mwisho ya kampeni ya “Ikiingia Tu Goli” itafanyika wiki hii, ambapo mshindi mmoja atajishindia Shilingi milioni 50.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya tisa ya kampeni hiyo inayofanyika kwa ushirikiano na Hisense, Mkuu wa Idara ya Makampuni na Washirika – Mixx, Justine Lawena. amesema kampeni hiyo imeendelea kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma za kifedha kidijitali huku ikiwazawadia fedha taslimu na vifaa mbalimbali.

Katika droo hiyo, washindi 10 wamepatikana, ambapo saba wamejishindia Shilingi milioni moja kila mmoja, huku watatu wakijishindia vifaa vya Hisense.

Lawena amesema, hadi sasa kampeni hiyo imewazawadia zaidi ya Watanzania 90 tangu ilipoanza.

“Fainali za Kombe la Dunia zimekwisha, lakini fainali ya kampeni yetu ndiyo inafuata wiki ijayo. Hapo ndipo tutampata mshindi wa Shilingi milioni 50. Bado kila Mtanzania ana nafasi ya kushinda kwa kutumia Mixx Super App,” amesema Lawena.

Amesema, ili kushiriki droo ya mwisho, mteja anatakiwa kutumia Mixx Super App kufanya miamala kama kutuma na kupokea fedha, kulipa bili na kufanya malipo ya Serikali.

Lawena amewataka wateja kuwa makini wanapopigiwa simu kutoka namba 100, akieleza kuwa hiyo ndiyo namba rasmi ya kuwataarifu washindi.

“Tunawakumbusha wateja kupokea simu kutoka namba 100. Usipoipokea unaweza kupoteza fursa ya kuthibitisha ushindi wako. Bado una nafasi ya kushinda kwa kuendelea kutumia Mixx Super App,” amesema.

Mmoja wa washindi wa Shilingi milioni moja, David Kisusi, amesema ushindi huo umempa motisha zaidi kuendelea kutumia Mixx kutokana na urahisi na usalama wa huduma zake.

“Nimekuwa nikitumia Mixx kwa shughuli zangu za kila siku na ninaweza kulipia bili mbalimbali kwa urahisi kupitia simu yangu. Kinachonivutia zaidi ni usalama wa huduma hizi, kwani hata muamala unapokwenda kimakosa, kuna msaada wa haraka wa kuuzuia au kuurejesha,” amesema Kisusi. Kampeni ya “Ikiingia Tu Goli”, inayofanyika kwa ushirikiano kati ya Mixx na Hisense, inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali nchini huku mshindi wa mwisho akitarajiwa kujishindia Shilingi milioni 50.