June 14, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washindi ‘Kila muamala bao la ushindi’ wakabidhiwa zawadi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPUNI ya Mixx imewakabidhi zawadi washindi wa droo ya tatu ya kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi”, hatua inayokuja wakati hamasa ya michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™ ikiendelea kus8hika kasi.

Kampeni hiyo, inayofanyika kwa ushirikiano na Hisense yenye kauli mbiu ya “Ikiingia Tu Goli”, inalenga kuwapa watumiaji wa huduma za Mixx nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali wanapofanya miamala ya kila siku kupitia jukwaa hilo la fedha kidijitali.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo hivi karibuni mtangazaji na balozi wa kampeni hiyo, Meena Ally, amesema kampeni hiyo imeleta fursa ya kipekee kwa Watanzania kushiriki msisimko wa Kombe la Dunia huku wakinufaika na zawadi mbalimbali kutoka Mixx.

“Mpira wa miguu una nguvu ya kuunganisha watu, na kupitia kampeni hii Watanzania wanapata nafasi ya kushinda kila wanapofanya miamala yao ya kila siku. Mimi niwahamasishe tu watanzania kuendelea kutumia huduma za Mixx kwa sababu kila muamala unaweza kuwa bao la ushindi na kubadilisha maisha yako,” amesema Meena Ally.

Katika droo ya tatu ya kampeni hiyo, washindi saba wamejishindia fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja na wengine watatu wakiondoka na zawadi kutoka Hisense ikiwemo Friji, TV ya inchi 55 na Spika ya muziki.

Mmoja wa washindi wa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja, Masudi Sauko, mjasiriamali na mkazi wa Dar es Salaam, amesema zawadi hiyo itakuwa msaada mkubwa kwake katika kuendeleza shughuli zake za kiuchumi na familia yake.

“Ninafuraha sana kuwa miongoni mwa washindi wa kampeni hii. Fedha nilizopata zitaniwezesha kuongeza mtaji katika biashara zangu za ujasiriamali na pia zitanisaidia kulipia ada ya mtoto. Lengo langu ni kushinda zawadi kuu ya Kampeni kwahiyo bado ntaendelea kutumia huduma za Mixx ikiwemo kufanya miamala na huduma ya Lipa kwa Simu.” amesema Sauko.

Bado wapo washindi watano wa kampeni ambao watapata nafasi ya kusafiri kwenda Mexico kushuhudia mechi za Kombe la Dunia la FIFA 2026™ mubashara pamoja na mshindi mmoja wa zawadi kuu ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa kampeni.

Kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi” pia inalenga kuhamasisha matumizi ya Mixx Super App kupitia huduma mbalimbali ikiwemo kutuma fedha, kulipa bili, kufanya malipo kwa njia ya Lipa kwa Simu na miamala mingine ya kila siku.

Mixx imewahimiza Watanzania kuendelea kushiriki kampeni hiyo kwa kutumia huduma zake, ikieleza kuwa kila muamala unaofanyika unatoa nafasi ya kuingia kwenye droo za ushindi.