


Na Mwandishii wetu
MABALOZI wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania leo, Juni 19, 2026, wameanza safari kuelekea Jijini Dodoma kwa kutumia Treni ya Kisasa ya Mwendokasi (SGR) kushiriki Grand Bunge Bonanza litakalofanyika Juni 20, 2026 katika Uwanja wa Jamhuri.
Bonanza hilo linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha umoja, ushirikiano na uhusiano wa kimataifa kupitia michezo, huku likiwa sehemu ya maandalizi na hamasa kuelekea mashindano ya AFCON 2027, ambayo Tanzania itaandaa kwa ushirikiano na Kenya na Uganda.
Mabalozi waliosafiri ni wa nchi za Comoro, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Afrika Kusini, Sudan, Zimbabwe, Msumbiji na Angola.
Ushiriki wa mabalozi hao unaonesha namna michezo inavyoendelea kuwa chombo muhimu cha kuunganisha mataifa, kuimarisha diplomasia na kujenga mahusiano imara kati ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Grand Bunge Bonanza linatarajiwa kukutanisha viongozi wa Serikali, wabunge, mabalozi na wadau mbalimbali wa michezo katika tukio litakalobeba ujumbe wa mshikamano, urafiki na ushirikiano wa kimataifa, sambamba na kuhamasisha maandalizi ya AFCON 2027.

More Stories
WRRB yatoa fursa mpya kwa wafugaji
Mkurugenzi NEC Mfumo PBPA
Waajiri wanaozingatia sheria za kazi wapongezwa