April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Polepole awatakia heri wachezaji wa gofu Lugalo

Na Mwandishi Wetu

BALOZI wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole amewatakia heri Wachezaji wa gofu kutoka klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wanaoshiriki mashindano ya kuwaenzi Wanajeshi wa Malawi walipigana Vita ya Pili ya Dunia yatakayofanyika Uwanja wa Lilongwe nchini Malawi.

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea wachezaji hao wakiongozwa na Meja Jenerali Ibrahim Mhona alisema Mashindano hayo ya kuwaenzi Maveterani waliopigana Vita ya Dunia ya pili lakini pia yanadumisha Ujirani mwema.

“ Najua mashindano haya ni ya kuboresha ujirani mwema lakini kuibuka na ushindi ni Muhimu katika kutekeleza falsafa ya mashindano ambayo kushinda kwa wachezaji ni faraja .”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu amesema timu yake iko vizuri na wanaamini watacheza vyema.

“ Walipokuja Tanznai kwenye Kombe la Mkuu wa majeshi tuliwashinda hivyo tunaamini nao wanataka kufanya Vizuri nyumbani lakini nasi tumejiandaa kucheza mchezo mzuri”.

Kwa Upande wake Nahodha wa Timu ya Golf ya Jeshi la Malawi Brigedia Jenerali Kondwani Kalino amesema amefarijika kwa Timu ya Tanzania kufika na wanatarajia kuanza na mashindano ya Kijeshi baina ya Timu hizo Mbili.

“ Siku ya kwanza ya Mashindano tutashindana jeshi la Malawi na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania yaani Combat Fidle na siku ya Pili tutacheza Shindano la kuchangia fedha kwa Ajili ya wananjeshi wa Malawi waliopigana Vita ya pili ya Dunia ambapo Mgeni rasmi ni Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwela.”

Ujumbe wa wachezaji wa Tanzania watakaoshiriki Mashindano hayo ni Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Witara,Meja Jenerali Ibrahim Mhona,Brigedia Jenerali Mstaafu Julius Mbilinyi, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwogo.
Wengine ni Kanali Martin Msumali, Meja Japhet Masai, Meja Selemani Semunyu, Kapteni Samwel Mosha, Kapteni Chediel Msechu na Koplo Malius Kajuna aliyeibuka Mshindi katika mashindano ya awali Mwaka huu Nchini Tanzania.