April 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mabaki ya shule ya Msingi Byamungu iliyoteketea kwa moto mkoani Kagera

BAKWATA yatoa tamko zito majanga ya moto mashuleni

Asimwe clemence asimweclemence@gmail.com

Na Irene Clemence

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeagiza wamiliki wote wa shule nchini na viongozi wao kuimalisha ulinzi ndani ya shule zao sambamba na kuchukua tahadhari za kina.

Pia imezitaka shule hizo kuimarisha miundombinu ya mashule ikiwemo mifumo ya umeme, uzio wa shule pamoja na kuhakikisha kunakuwa na vifaa vya zimamoto

Rai hiyo imetolewa na BAKWATA kutokana na kuwepo kwa mfululizo wa matukio ya kuungua kwa moto kwa shule mbalimbali nchini, ikwemo hivi karibuni shule ya msingi ya Byamungu iliyopo Wilaya Kyerwa mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi alisema BAKWATA ilipokea taarifa za masikitiko juu ya janga la moto lililotokea mkoani Kagera Septemba 14 katika shule ya Msingi Byamugu.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo alituma ujumbe wa viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Kagera ambao ulikuwa ukiogozwa na Katibu mkoa.

“BAKWATA inatoa pole kwa shule ya msingi uongozi Byamungu,wazazi waliofiwa na watoto wao, watoto waliojeruhiwa katika ajali hiyo pamoja na Rais John Magufuli, Waziri wa Elimu, pamoja na mkuu wa shule,”amesema Sheikh Zuberi

Amesisitiza kuwa BAKWATA itaendelea kusubiri taarifa rasmi ya vyombo vya usalama juu ya matukio mbalimbali yaliotokea ikiwemo hili la mkoani Kagera.

“Tume iliyoundwa bado inaendelea na uchaguzi tuna imani wakimaliza watatuletea taarifa juu ya matukio haya,”amesema

Ameoongeza kuwa mpaka sasa idadi ya shule saba zilipatwa na majanga ya moto na kwamba BAKWATA itaendelea kusubiri taarifa rasmi.

Aidha amewaomba Waislamu wote nchini kwa ujumla kuendelea kuwa na subira katika kipindi hiki chote . Pia aliwasii wananchi kwa ujumla kuendelea kuilinda amani iliyopo.

Katika hatua nyingine, Sheikh Zuberi amewaomba wazazi wote kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki na kuendelea kuwapeleka watoto wao mashuleni .