October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zuchu atembelea kisiwa cha gereza Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hapa nchini kwa upande wa wanawake kutoka WCB, Zuhura Othman Soud maarufu kama ‘Zuchu’leo amepata fursa ya kutembelea kisiwa cha Gerza kinachojulikana kama Kisiwa cha Changuu kilichipo kwenye mji Mkongwe, Visiwani Zanzibar.

Zuchu ametembelea Gereza hilo ikiwa mongon mwa ziara zake kabla ya kufanyika kwa shoo yake kubwa ujulikanayo Zuchu Homecoming na Zantel itakayofanyika Agosti 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Amani kisiwani humo.

Akizungumzia Kisiwa hicho kupitia Ukurasa wake wa Instagram Zuchu amesema, kutoka Mji Mkongwe hadi kufika kisiwani hapo ni mwendo wa dakika 30 kwa mashua.

“Kisiwa cha Changuu kilitumika kama gereza la watumwa waasi na masultani kutoka miaka ya 1860 hadi mwisho wa biashara ya watumwa.

“Siku hizi kisiwa hukupa nafasi ya kutoroka kwa amani na utulivu. kisiwa hiki ni nyumba ya kobe wakubwa wa ardhi ambao waliletwa kutoka Seychelles katika karne ya 19.

Ziara huanza saa 9:00 asubuhi hadi 3:30 jioni, hapo utaweza kuona kobe kubwa, viumbe wazuri wa baharini, miamba ya matumbawe na pia ni tovuti bora ya kufanya Snorkeling,” amesema Zuchu.