October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizkid avunja rekodi mauzo ya tiketi London

LONDON, England

MKALI wa muziki kutoka nchini Nigeria, Wizkid

ameutaarifu umma kuwa tiketi ambazo zitatumika

katika shoo yake inayotarajiwa kufanyika nchini

Uingereza Novemba 28 mwaka huu zimemalizika mapema.

Nyota huyo amethibitisha Taarifa hizo za kumaliza

kwa tiketi za show yake kupitia kwenye Ukurasa wake

wa Instagram ambapo ameandika…….”Sold out the O2 in

12mins!! Love u london!!,” amesema Wizkid

Miongoni mwa nyimbo zake zinazofanya vizuri kwasasa

kwenye charts mbalimbali ni huu uitwao ‘Essence’

aliyomshirikisha Tems ambao kupitia mtandao wa

Youtube umetazamwa na watu zaidi ya 19,206,422.