January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mr Blue: Nilifanya Shoo Mombasa nikalipwa Simu

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Khery Sameer Rajab maarufu kama ‘Mr. Blue’ amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya kitu ambacho hatokisahau kitendo cha kufanya shoo Mombasa na kulipwa ujira wa simu mwaka 2004.

Akizungumzia hilo, Mr. Blue amesema alifanya shoo ya nguvu ambayo iijaza watu jambo ambalo hakulitegemea hata kidogo ukizingatia alikuwa mdogo.

“Katika vitu ambavyo siwezi kuvisahau vya huzuni na vyakufurahisha ni kitu kimoja cha furaha ambachi siwezi kukisahau, niienda Mombasa kufanya shoo mwaka 2004, aliyenipeleka kwa ajili ya kufanya shoo hiyo alinilipa simu maana nilikuwa mdogo sanaakaniambia wewe twende kama unaenda kusalimia, lakini kufika kule nikakuta shoo kubwa sana kitu ambacho sikutegemea.

“Imefika muda wa shoo nikakuta watu wengi sikujua kama watu wote walikuja kwa ajili yangu, mimi nilijua kuwa watu wale walikuja kwa kitu kingine halafu ndio nifuate mimi. Kilichofuata baada ya kufika pale mimi nikaanza kulia kilio kikubwa, wakawa wananiuliza Shida ni nini?, nikasema haiwezekani hawa watu wote wananisubiria mimi kwenda kuimba.

“Siwezi kuwaimbia watu wote hawa, nafikiri ni kwasababu ya ule umri niliokuwa nao pamoja na ule Uoga, lakini niliweza kwenda kuimba na ile Shoo ni Shoo siwezi kuja kuisahau kwenye maisha yangu,” amesema Mr. Blue.