March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wauza sukari watahadharishwa kupandisha bei Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Na Mwandishi Wetu TimesMajira Online

KATIKA Kuelekea katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi April Wafanyabiashara, wauzaji  wa sukari Nchini wametakiwa kutokubadisha bei ya bidhaa hiyo ili kuondoa  adha kwa wananchi na waumimi wanaofunga katika mwezi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam juzi Mkuu wa Idara ya Biashara kutoka Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Fimbo Butallah amesema upandaji wa bei wa bidhaa ya sukari umekuwa ukiwakandamiza watumiaji wa sukari kutokana na matumizi yake kuongezeka zaidi katika mfungo wa Ramadhani.

Amesema katika kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana Kampuni hiyo imejidhatiti kuhakikisha kuwa walaji wa bidhaa hiyo wanaipata kwa wakati kwa bei nzuri

Butallah amesema tamko la kuwataka Wafanyabiashara kutokupandisha bidhaa ya sukari limekuja kutokana na kuwepo kwa  historia ya kupanda kwa bei za bidhaa nyingi za vyakula kila uanzapo mfungo upelekea kusababisha adha kubwa kwa Wananchi hususani waumini wanaofunga katika mwezi huo.

“Sisi kama wazalishaji sheria aituruhusu kuwapangia Bei wauzaji  wa bidhaa hii kinachoruhusiwa ni kumpatia bei yako na kumpendekezea bei za yeye kuuza tunafahamuwa soko huria sisi kama wazalishaji wa sukari atujapandisha bei ya bidhaa hiyo ..tunawaomba wafanyabiashara kote nchini kutokupandisha bei katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuepeka taharuki”amesema

Na kuongeza

“Kwa sasa sukari inatikana hakuna taharuki tunachoogopa ni pale mwezi unapoanza tunaanza kuona taharuki ya kupanda kwa bidhaa hiyo.

Aliongeza kuwa wao kama wasambazaji wa bidhaa hiyo wameona wanaowajibu mkubwa wa kuwashauri wafanyabiashara kuhusu upandaji holela wa bei hasa pale wanapokuwa awajapandisha bei ya bidhaa hiyo.

Hata hivyo amesema  kampuni h Kilombero inayo akiba ya kutosha ya Sukari ya kulivusha taifa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo tayari wamepata kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ili kuziba pengo la uzalilishaji.

“Tayari tumekwishaanza taratibu za uagizaji wa sukari ambayo inatarajia kuanza kuingia nchini mda wowote kuanzia sasa tunawaomba wananchi wasiwe na hofu kuhusu upandaji holela wa bei ya Sukari hususani bwana sukari kwani kampuni imeandaa mikakati thabiti ya kukabiliana na tatizo hili katika msimu wote”amesema

Aidha amesema katika historia yao ya mauzo  katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kampuni hiyo imekuwa ikiuza tani bidhaa ya sukari zisizozidi elfu 13000 .

Mbali na kuuza bidhaa hiyo pia kampuni hiyo imesema  tayari inayostoku ya   ya tani elfu 20 ya sukari  ambayo itaweza kukidhi mahitaji ya sukari katika nchi.