June 28, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waokaji watakiwa kujiunga na ushirika

Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online- Mwanza

WATAALAMU wa sekta ya kuoka keki mkoani Mwanza,wamehimizwa kujiunga na vyama vya ushirika ambavyo vitawasaidia kupata masomo,fursa za kifedha pamoja na kukuza biashara zao.

Hayo yameelezwa Juni 26,2026 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda wakati  akiongoza kikao cha waokaji wa keki wa mkoa huo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ambapo amesema,ushirika ni njia muhimu ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa sekta moja, kuwafanya watambulike rasmi, kuwa na ofisi na kurahisisha uratibu wa shughuli zao pamoja na kuandaa maonesho ya bidhaa zao.

Huku amewasisitiza  umuhimu wa kudumisha amani,ambapo alieleza kuwa hakuna biashara inayoweza kustawi bila mazingira ya amani. 

“Waokaji wa keki mnapaswa kuishi kwa kuheshimiana,kushirikiana na kudumisha uhusiano mwema ndani ya familia na maeneo yenu ya kazi,”amesema Mtanda 

Kwa upande wake Mratibu wa kikao hicho kutoka Kampuni ya BJ Entertainment,Benard James amesema, sekta ya uokaji inakua kwa kasi, jambo lililowasukuma kuandaa maonesho maalumu ya waokaji ili kuwapa fursa ya kutangaza bidhaa zao na kupanua masoko.

Naye  Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mwanza Hilda Boniphace amesema,kikao hicho ni sehemu ya maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ya kuwahamasisha makundi mbalimbali kujiunga na ushirika ili kunufaika na fursa za mikopo, masoko na maendeleo ya kiuchumi.

Hivyo ameataka waokaji keki kuongeza ubunifu,kuimarisha ubora wa bidhaa zao na kutafuta masoko mapya ili kukuza biashara na kuongeza ushindani.

Akisoma risala ya Umoja wa Waokaji, Emmanuel Masanja amesema,waokaji wa Mkoa wa Mwanza wamejipanga kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza sekta hiyo huku wakitarajia kupata ushirikiano zaidi kupitia mfumo.