Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online- Mbeya
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ndele Mwaselela, ameungana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe kuwatembelea wafanyabiashara 35, wakiwemo mama lishe na baba lishe, waliopoteza vibanda vyao vya biashara kufuatia janga la moto lililotokea Kata ya Kimo.
Akiwa ameambatana na viongozi wa CCM wilayani humo Juni 27,2926 Mwaselela alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Rungwe Antony Mwantona,kwa jitihada za kuwasaidia wananchi wenye uhitaji na kwa kushiriki katika upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara walioathirika na moto.

Mwaselela amewataka wanachama wa CCM kuendelea kujibu vyama vya upinzani kwa hoja pamoja na kumtetea Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Mmejionea wenyewe kwamba tumepatwa na janga la moto,lakini wapo ambao hawajajitokeza hata kutufariji badala yake wameendelea kutukosoa. Sisi CCM si kwamba tuna fedha nyingi, bali kinachotuongoza ni upendo ambao ndiyo msingi wa chama chetu,”amesema Mwaselela.
Sanjari na hayo ametoa pole kwa wananchi wa Rungwe walioathiriwa na majanga mbalimbali na kukabidhi mitaji iliyochangwa na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya, Ofisi ya Mbunge wa Rungwe pamoja na yeye binafsi kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Hata hivyo amewapongeza viongozi wa CCM wilayani Rungwe kwa kuendelea kuimarisha chama na kudumisha mshikamano,Mbunge Antony Mwantona kwa ushirikiano wake na kwa kuendelea kuwa karibu na wananchi hususani katika kipindi hiki cha kuwafariji na kuwainua waathirika wa janga la moto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rungwe, Meckson Mwakipunga,ametoa pongezi kwa viongozi ikiwemo Mkuu wa Wilaya kwa kuwa karibu na waathirika wa janga hilo pamoja na Serikali kwa kuwawezesha baadhi ya waathirika kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, huku wakipewa nafuu ya muda wa marejesho.
​

More Stories
Juhudi zasaidia kupunguza uingizwaji bidhaa za magendo
Waokaji watakiwa kujiunga na ushirika
Zambia yapongeza mafanikio ya Tanzania Sekta ya Umeme