March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uchangiaji damu kwa hiari

Mwamko wa uchangiajia damu waongezeka nchini

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

ONGEZEKO la uchangiaji wa damu katika kitengo cha damu salama, kilichopo chini ya Wizara Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto umeendelea kuridhisha tofauti na miaka mingi ya iliyopita.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma jana na Henry Mchete, ambaye ni mhamasishaji wa uchangiaji damu kwenye kitengo cha afya.

Mchete amesema mpango wa uhamasishaji ndio umeweza kupata mafanikio ya utoaji mazuri ya uchangiaji damu. Amesema wamekuwa wakitoa elimu ya uchangiaji damu kwa njia mbambali, ikiwemo kutumia vyombo vya habari.

“Hapo mwanzo tulikuwa kunakimbiwa kukimbiwa na wananchi wengi pindi tulipokuwa kujitokeza kuomba uchangiaji wa damu kwa wananchi hasa vijijini, kwani walikuwa na hofu kubwa kwa dhana ya unyonyaji damu, lakini kwa wakati huu wamefunguka na uelewa ni mzuri,” amesema Mchete.

Mhasishaji huyo amesema ongezo hilo la utoaji damu, lilionekana kwenye uzinduzi wa wajasiriamali uliyoitwa; “Mwanamke shujaa.”
Katika uzinduzi huo watu wengi kwa kipindi kifupi hicho walichangia damu watu 92 kwa siku tatu. Amesema uchangiaji wa utoaji wa damu, mtoaji anakuwa na vigezo vinavyotakiwa, kama vile afya, uzito, kiwango damu na pia kuangalia uwezo wa utoaji.

Aidha amesema kuna changamoto ya ufinyu wa vifaa vya vipimo kwani ni vichache na vilizopo ni vile vya upimaji damu, msukumo wa damu, kisukari, kifua kikuu na kifafa.

Mchete amefafanua kuwa uhaba huo hauathiri hatua za utoaji wa damu, lakini iwapo vitakuwepo vifaa vingi inasaidia zaidi katika zoezi hilo.