Na Judith Ferdinand,Mwanza
AWAMU ya pili ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto wenye mwenye umri chini ya miaka 10,linatarajia kufanyika kwa siku nne Mei 7 hadi 10,2026,ambapo Halmshauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza inatarajia kuwachanja takribani watoto 176,644.
Zoezi la utoaji wa chanjo ya polio awamu ya pili litahusisha watoto wote waliopatiwa chanjo awamu ya kwanza na wale na ambao hawakupatiwa.

Hivyo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi halmshauri hiyo kupitia idara ya afya imetoa elimu ya chanjo ya polio na madhara yatokanayo na ugonjwa huo kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wazee maarufu, wamiliki wa shule binafsi na viongozi wa vijana.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Kalunde Gisema,amesema mafunzo hayo yakilenga kutoa uelewa kwa jamii kupitia viongozi hao juu ya umuhimu wa chanjo ya polio noVP2 awamu ya pili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 10.
“Hawa ni watu muhimu wanaoaminika na kusikilizwa katika jamii,hivyo kupitia mafunzo hayo tunaamini sehemu kubwa itapata uelewa juu ya umuhimu wa chanjo ya polio awamu ya pili.Pia itahamasikana watoto wao kupata chanjo hivyo kuwakinga na virusi vinavyoeneza ugonjwa wa polio,”amesema Kalunde.

Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Ilemela,Abdulmalick Juma,ameahidi kutoa elimu hiyo waliopata kwa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo kwa watoto na kuhamasisha wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo ya polio.
Katibu wa soko la Kiloleli wilayani Ilemela mkoani Mwanza,Happynes Lakate,amesema atahakikisha anawahamasisha wafanyabiashara wa sokoni hapo na masoko jirani wenye watoto wa umri chini ya miaka 10, kuhakikisha wanapata chanjo hiyo ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.
Ambapo amesema mtoto akipata maradhi mzazi hataweza kufanya biashara ajatjikita zaidi kuhakikisha mtoto wake anapata tiba na hivyo uchumi kushuka.


More Stories
MWADETA yahamasisha matumizi ya folic acid
DC ubungo awaasa zimamoto kushirikiana na wadau wengine
RC Shinyanga awaalika wananchi kupata msaada wa kisheria