Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
JESHIi la Zimamoto na Uokoaji limetakiwa kushirikiana na Wakala wa barabara Mijini na Vijijini(TARURA) pamoja na shirika la ugavi wa umeme Nchini (TANESCO)katika ujenzi wa barabara na uunganishaji wa umeme ili pindi inapotokea majanga ya moto kuwa rahis kuwezai kuyadhibiti.
Agizo hilo limetolewa Mei 4,2026 na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Zimamoto Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
“Hakikisheni TARURA wanapojenga barabara mshirikiane nao ili kurahisisha Miundombinu ya barabara inapitika kirahisi pindi inapotokea majanga ya moto, amesema”.DC Msando.
Nakuongeza kuwa”pia TANESCO mshirikiane nao katika uunganishaji wa mifumo ya umeme kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo masoko na maduka ili kuwa na mifumo imara ya kufikika mara majanga ya moto yanapotokea.

DC Msando ameongeza kuwa Zimamoto wanatakiwa kujiridhisha ubora wa vifaa vinavyotumika kuunganisha umeme kwenye masoko na maduka,na endapo watabaini vifaa hivyo haviko salama,aliyeunganisha huduma hiyo ya umeme achukuliwe hatua za kisheria.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji Tanzania na msemaji wa jeshi hilo DCP Puyo Nzalayaimisi ameishukuru Serikali kwa kulipatia magari na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuzimia mioto na kufanya Uokoaji pindi majanga yanapotokea.
“Tunashukuru sana Serikali ya Dkt.Samia Sululu Hassan kwa kuliborsha Jeshi letu kwa kutupatia vifaa vya kisasa,na sisi tunaendelea kujitoa kwa moyo wa dhati katika kuwahudumia Wananchi”amesema.
Awali Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Kizimamoto Ilala SACF Mabusi Peter amesema kuwa sasa wapo kwenye mchakato wa kufungua vituo vingine vinne vya Zimamoto katika maeneo ya Kinyerezi,Kivule,Masaki na Kigamboni.
Pia amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea kushirikiana vizuri na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa washirika wa Zimamoto,nakwamba kwasasa Jeshi hilo lina wadau wa kujitolea wapatao 75, pia klabu 50 zenye Wanachama 1000.

More Stories
RC Shinyanga awaalika wananchi kupata msaada wa kisheria
Rais Dkt.Samia akutana na Drogba
Rais Ruto Aitambua Tanzania kama Kitovu cha Nishati Afrika Mashariki