Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOline
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga,Mboni Mhita, amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kupata huduma za msaada wa kisheria zitakazoanza kutolewa kesho tarehe 6 hadi 20 Mei 2026 katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga.
Mhita ametoa wito huo leo tarehe 5 Mei 2026 akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Shinyanga, akisisitiza kuwa huduma hizo zinatolewa bila malipo yoyote kwa wananchi wote kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili, na kwamba zitapatikana katika halmashauri zote za mkoa kwa muda wote wa kampeni hiyo.

More Stories
Yas yazindua Mnara wa 5G Masasi
Wafanyabiashara wahimizwa kutumia nembo ya Tanzania
Tozo ya mafuta yaboresha barabara Mwanza