Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online- Mwanza
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade),imewahimiza wafanyabiashara kutumia nembo ya Taifa ya Tanzania ili kuongeza thamani katika bidhaa zao.
Hayo yameelezwa Agosti 2,2026 na Msimamizi wa Ofisi ya Tantrade Kanda ya Ziwa,Ofisa Mwandamizi Cecilia Mwandepa,katika uzinduzi wa maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi,yanayofanyika katika viwanja vya Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza,wakati waandishi wa habari walipotembelea banda la mamlaka hiyo.
Mwandepa amesema,kauli mbiu ya maonesho hayo inasema,”Tambua soko,ongeza tija kutekeleza dira 2050″ huku akisisitiza namna utumiaji wa nembo hiyo unavyoweza kusaidia wafanyabiashara kufikia soko kwa urahisi.
Ambapo ametaja moja ya faida ya kuwa na alama hiyo ni pamoja na kutambulisha bidhaa ya mfanyabiashara husika katika soko na kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania pamoja kujenga uzalendo wa matumizi ya bidhaa za hapa nchini.
“Sisi TanTrade,tumetambua soko lipo na vitu muhimu vinaohitajika katika soko moja wapo ni nembo ya Taifa ya Tanzania,ambayo hii ni alama inayotambulisha bidhaa zetu katika soko la ndani na nje,”amesema Mwandepa.
Sanjari na hayo ametaja baadhi ya vigezo ili kupata alama hiyo ni kuwa biashara ilio sajiliwa,iwe bidhaa inayozalishwa nchini Tanzania naimezingatia vigezo vyote kisha wataenda TanTrade kupitia njia ya kidigitali.
“Tunahamasisha sasa wazalishaji kuweza kutumia nembo yetu kwa sababu inakujengea uaminifu na hadhi lakini na pia inaonesha ubora wa hiyo bidhaa.Tunahamasisha Watanzania kuwa wazalendo kwa kuweza kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini,”amesema Mwandepa.
Hata hivyo amesema,kwa kufanya hivyo kupitia viwanda vilivyopo hapa nchini vitaongeza uzalishaji ambao utaongeza ajira na kuchangia pato la Taifa.

More Stories
Tozo ya mafuta yaboresha barabara Mwanza
Millya:Ongezeni upatikanaji wa mbolea kwa ajili ya uzalishaji
Rungwe yaendelea kutatua changamoto za wakulima wa parachichi