April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme

Mgombea ubunge ACT Wazalendo Kigamboni aanika vipaumbele

Na David John timesmajiraonline

WANANCHI wa Kigamboni jijini Dar es Salaam wameshauriwa kuchagua Chama cha ACT-Wazalendo kama kweli wanahitaji maendeleo ya kweli katika wilaya hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na mgombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tungi Mnadani jimboni humo.

Amesema miaka zaidi ya 10 sasa jimbo hilo limekuwa chini CCM, lakini hadi sasa vijana wa Kigamboni karibu asilimia 79 hawana ajira rasmi, hivyo aliwaahidi kwenda kusimamia haki za wavuvi.

“Nawaomba ndugu zangu mnichague kwani shida zenu nazijua na ni za miaka mingi, ikiwemo sekta ya uvuvi, ukosefu wa ajira kwa vijana, mikopo kwa akina mama na huduma Bora za Afya.

Haya yote mkinichagua nitakwenda kuyashughulikia.”amesema Mwanaisha

Ameongeza kuwa kigamboni kunachangamoto ya makazi Bora hivyo Kama watamchagua atatumia elimu yake ya uwanasheria na kushirikiana na watu wa mipangomiji, na mazingira kuhakikisha wanapima Ardhi ili wananchi wapate fursa ya kukopesheka.

Amesema kuwa miaka kumi ya mbunge aliyemaliza muda wake ni miaka ya changamoto nyingi Kwa wananchi wa Kigamboni na ndio maana hata yeye mwenyewe anakiri huku aliwataka ninyi wananchi mumchague tena ili akamalizie kazi .nakwamba wamkatae kwani hatoshi.

“Ndugu zangu Mimi ni biti mdogo lakini ni mwanasheria nawahakikishia mkinipa kura nakwenda kufanya mambo makubwa Kwa ajili ya Kigamboni yetu .si mnajua changamoto za Afya zilivyo madawa tatizo,lakini upande wa elimu madarasa machache katika shule zetu nitahakikisha mkinichagua tunakwenda kumaliza kero hii.”amesema

Amefafanua kwamba halmashauri zinatoa mikopo ya asilimia 10 kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya vijana, akina mama na walemavu, hivyi akichaguliwa atakwenda kuwabana ili walengwa wananufaike.

Kuhusu soko, amesema Wilaya ya Kigamboni Kwa muda mrefu imekosa soko la uhakika hali inayowalazimu wananchi kufuata huduma nje ya Kigamboni wakati maeneo ya wazi yapo, hivyo wakimchagua atashughulikia kero hiyo.

Aliwaomba wananchi hao ili mambo yaende vizuri basi wahakikishe wanampa kura diwani anayetokana na ACT-Wazalendo.