January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Abbasi awaongoza viongozi wa Afrika kushuhudia CANAF 2021

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas amewaongoza viongozi mbalimbali wa michezo wa mataifa ya Afrika kushuhudia mashindano ya soka yanayoendelea ya bara la Afrika CANAF 2021 jijini Dar.

Katika mechi ya Timu ya Kenya na Zanzibar, Kenya imeshinda magoli 5-0 dhidi ya Zanzibar katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Goli la kwanza na Nicholous Keiyo dakika ya 20 la pili dakika ya 23 na Mohamed Mungi la tatu dakika ya 33 na Augeni Makanga.

Goli la nne dakika ya 36 na mshambuliaji Diniel Safari wakati goli la 5 limefungwa na Albelt Mwakinga.

Hadi sasa timu ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa kufungwa zaidi ikiwa imefungwa jumla ya magoli 17 wakati yenyewe haijaambulia hata goli moja.