January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC kudhamini UDSM Marathon

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kufuatia mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Disemba 04, 2021 kuanzia na kumalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shirika la Bima la Taifa (NIC) wameingia mkataba wa makubaliano wa kudhamini mbio hizo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Yessaya Mwakifulefule amesema wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika sekta ya michezo kwa lengo la kukuza vipaji kwa watanzania na pia kujiepusha na magonjwa nyemelezi.

Amesema wataendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwasababu wamekuwa wadau wakubwa kwao katika biashara pia ndio kitivu cha elimu hapa nchini;

“Ni mara yetu ya kwanza kusapoti UDSM Marathon na haitakuwa mara ya mwisho kufanya hivyo, tutaendelea kushirikiana kama  ambavyo wamekuwa wadau wakubwa kwetu kwa muda mrefu”. Amesema Bw.Mwakifulefule.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa UDSM Marathon Lulu Kaaya amesema lengo kuu la mbio hizo ni kwaajili ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kuboresha maisha ya wanachuo;

“Lengo kuu la mbio hizi ni kwaajili ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kuboresha maisha ya wanachuo.”

Aliongeza kuwa “Kwasasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo katika ujenzi wa kituo cha wanafunzi (Student Center) inayojengwa kwenye Campus ya Mwalimu Nyerere Mlimani Jijini Dar es Salaam ambacho ni mahususi kwa kutoa mazingir mazuri ya mapumziko kwa wanafunzi”

katika mbio hizo wanatarajia kuwepo kwa mgeni rasmi ambaye atakuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia atashiriki kukimbia Kilomita 5.

Amesema mbio hizo zitakuwa na ruti kubwa tatu ambazo ni ruti ya Kilomita 21.1, ruti ya kilomita 10 na ruti ya kilomita 5 ambayo ruti hiyo mgeni rasmi atashiriki