May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Breaking News: Mtuhumiwa aliyemuua Beatrice Minja afariki Dunia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online Tabora

Jeshi la Polisi limesema mtuhumiwa Lucas Tarimio aliyekamatwa disemba 31,2023 kwa tuhuma za kumchoma visu na kusababisha kifo Beatrice Minja leo Januari 02,2024 amefariki dunia huko wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Akitoa taarifa hiyo leo Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msadizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesama kuwa mtuhumiwa huyo amefariki dunia huko Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kunywa sumu ya kuuwa wadudu wakati alipohisi kufikiwa na Mkono wa sheria.

Msemaji wa Jeshi hilo ameongeza kuwa taratibu nyingine za kisheria zinafuata kuhusiana na tukio hilo.