TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kufuatia Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda tarehe 18 Desemba, 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameivunja Bodi hiyo na amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Simuli.
Dkt. Nyansaho ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

More Stories
Yas yazindua Mnara wa 5G Masasi
Wafanyabiashara wahimizwa kutumia nembo ya Tanzania
Tozo ya mafuta yaboresha barabara Mwanza