April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zari awataka wanadamu kumuomba Mungu Kuhusu Corona

Zari awataka wanadamu kumuomba Mungu Kuhusu Corona

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MFANYABIASHARA na Mwanamitindo kutoka Uganda mwenye

makazi yake nchini Afrika Kusini ambaye pia mzazi

mwenzie, msanii wa Muziki wa Bongo fleva

Diamondplatnumz, Zari Hassan maarufu kama

‘zarithebosslady’, amewataka wanadamu kumuomba Mungu

kuhusu Ugonjwa wa Corona ambao kwa sasa umekuja kwa

kasi.

Akitoa rai hiyo kupitia kwenye Ukurasa wake wa

Instagram muda mchache uliopita Zari amesema, janga

hili la ugonjwa wa Corona halijaisha mpaka Mwenyezi

Mungu anapofunga pazia.

“Kila mtu mzuri, Ni ngumu kukaa kila mahali

na janga hili la

ugonjwa wa Corona bila ya kuchukua tahadhari kwani

halijaisha mpaka Mungu

atakapofunga mapazia, hivyo kaa

hapo ulipo kaa chini uombe kwa dini yako naamini Mungu

anaweza kutuepusha na balaa hili,” amesema Zari.