May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mjumbe wa kamati utendaji Yanga ambaye pia ni mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Eng Hersi Said (katikati), Makamu mwenyekiti wa Yanga David Mwakalebela na pamoja mtendaji mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingisa kulia wakitambulisha jezi mpya za Yanga 2020/21

Yanga yazindua rasmi jezi mpya

Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online

KLABU ya Yanga leo, imezindua rasmi jezi zake mpya kwa ajili ya kuzitumia katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021, mbapo za Kijani zitatumika ugenini na njano nyumbani.

Hata hivyo jezi hizo zimeanza kuuzwa leo, kwa Tshs 35,000 katika Makao makuu ya Klabu hiyo kwenye Duka maalumu la Klabu na Maduka ya Wadhamini wao, GSM.

Katika uzinduzi huo ambapo Mjumbe wa kamati utendaji Yanga ambaye pia ni mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Eng Hersi Said ndiye aliyezindua huku wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wakishuhudia tukio hilo.

Mara baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba ambao ni wadhamini wakuu wa klabu ya Yanga, amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua jezi halisi ili kuiongezea pato klabu hiyo.

Tarimba pia amewataka Yanga, kuwapa furaha mashabiki wao hasa kutokana na juu ya mafanikio ya klabu hiyo katika suala zima la usajili walioufanya msimu huu.

“Niwatakie kila lakheri Yanga, bila shaka na klabu nyingine katika ligi hii ambayo imeanza majuzi, na ninachotaka kimoja niseme ni kwamba wapeni furaha wapenzi wenu, wapeni furaha wananchi juu ya mafanikio ya Klabu hii kutokana na usajili na haya mambo mengine yanayofanyika,” alisema Tarimba.