April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,(TMF),Fausta Musokwa akiongea na waandishi wa habari.

Watumiaji wa barabara waendelea kupewa elimu ya usalama barabarani

Na Penina Malundo,TimesMajira,Online

KAMISHNA Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Mkadam Khami amesema katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu jumla ya shule 5,320 na wanafunzi 592,396 wamepatiwa elimu  juu ya usalama barabarani huku vijiwe vya bodaboda 11,760, madereva  wa bodaboda  212,464 wamepatiwa elimu hiyo.

Pia takribani stendi za Mabasi 3,589 zilifikiwa katika utoaji wa elimu hiyo, mabasi yakiwa  1,182,366 na i abiria 6,874,225 walipata elimu  ya usalama barabarani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Kamishna

Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Mkadam Khami  wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na  Ajali za Barabarani,ikienda sambamba na utoaji wa vyeti kwa wachora katuni waliotoa mchango wao katika uchoraji wa katuni kuelimisha jamii.

Amesema jeshi hilo limekuwa likikazia  usimamizi wa Sheria ya usalama barabarani kwa kufanya operesheni mbalimbali za usalama barabarani na kuhakikisha linatoa elimu ipasavyo kwa watumiaji wa barabara.

ACP,Khami amesema wamekuwa wakijitahidi  kuthibiti makosa hatarishi kama vile mwendo kasi, kupima ulevi, kusimamia madereva kufuata michoro ya barabarani.

“Tumekuwa tukiitumia mihadhara mbalimbali  kama maadhimisho  ya nikita nenda kwa usalama barabarani  katika maonyesho kama ya saba saba na ya nane  nane  kutoa elimu,”amesema na kuongeza

“Teknolojiaya habari na Mawasiliano imekuwa ya msaada mkubwa katika kuhakikisha kwamba madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani wanadhibitiwa,”amesema

Aidha amesema katika kukazia usimamizi wa sheria wamekuwa wakifanya operesheni mbalimbali za uslama barabarani kudhibiti makosa hatarishi yakiwemo mwendokasi,kupima ulevi,kusimamia madereva kufata michoro ya barabarani.

Mkurugenzi  wa Mpito wa Tanzania Media Foundation,(TMF),Fausta Musokwa amesema uandishi wa habari wenye maslahi kwa umma unaweza kusaidia  kuimarisha usalama barabarani.

“TMF ni taasisi inayofanya kazi kuimarisha uandishi wa habari wenye maslahi kwa umma na kushirikiana na wadau mbalimbali  ili kujenga uwezo katika sekta ya habari Tanzania, “amesema

Amesema habari za usalama barabarani zimechangia kuboresha usalama barabarani na kumgusa  kila mmoja imemgusa na kubadilishana mtazamo wa watu na kupaza sauti  lengo likiwa kuokoa maisha yao.

“Leo siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao  kutokana na ajali za barabarani ni  vema kutambua usalama barabarani ni vyema  waandishi wa habari kuzingatia sheria na misingi ya uandishi kwa kushirikiana na Polisi ili kupata taarifa sahihi na kutoa haki ya kujibu,”amesema