Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na African Feature Foundation na Global Image Care kutoka Korea Kusini, inatarajia kufanya kambi maalum ya upandikizaji wa figo na urekebishaji wa mishipa ya kuchuja damu kwa wagonjwa wenye changamoto ya figo kuanzia tarehe 15 hadi 19 Agosti 2026.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya kambi hiyo, Dkt. Daud Katwana, Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Muhimbili-Mloganzila, amesema hospitali hiyo inatarajia kufanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa wanne (4), pamoja na kurekebisha mishipa ya kuchuja damu kwa zaidi ya wagonjwa 50.

Kwa mujibu wa Dkt. Katwana, kambi hiyo itatoa fursa kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo kupata huduma zinazohitajika bila kulazimika kusafiri nje ya nchi kwenda kufuata matibabu hayo.

More Stories
TANESCO yabaini matukio ya Wizi wa Umeme Kinondoni
DCEA yazindua klabu kupinga dawa za kulevya vyuoni
Serikali yaimarisha uhimilivu bei za mafuta nchini