April 23, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania wang’ara Yas Kill Intenational half Marathon 2026

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

WANARIADHA  wa Kitanzania wameendelea kung’ara katika ardhi ya nyumbani, kupitia mbio za kilomita 21 maarufu ‘Yas Kili International Half Marathon 2026’.

Mbizo hizo zinazofanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro ni moja ya matukio makubwa ya michezo barani Afrika.

Akizungumza wakati wa kuwapongeza washiriki, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amessema mbio za mwaka huu zimeonyesha namna Watanzania wanavyoinuka na kuthibitisha uwezo wao katika riadha.

“Kile kilichofanyika Moshi leo sio tu mashindano; ni uthibitisho wa kujituma, uzalendo na uwezo mkubwa wa Watanzania kushindana na kuibuka na ushindi,” amesema Makonda.

Makonda pia amewasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliahidi kuwa mgeni rasmi kwa mashindano ya Kili Marathon kwa mwaka ujao huku.

Lakini pia,  ameahidi kuongeza dau nono la shilingi milioni 100 za kitanzania kwa washindi.

“Yas Kili International Half Marathon imeendelea kuwa jukwaa muhimu linalounganisha watu, kukuza utalii na kuleta hamasa mpya katika sekta ya michezo nchini.”Amesema.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton Bacara, amesema ushindani ulioonekana katika mbio za kilomita 21.1 umedhihirisha ubora wa wanariadha wa Tanzania na nguvu ya hamasa inayozidi kukua kila msimu.

Bacara amesema, udhamini wa zaidi ya miaka 12 wa kipengele cha Yas Half International Marathon unatokana na dhamira ya Yas kuwa mshirika wa maendeleo ya michezo nchini.

Kaulimbiu ya mwaka huu ya “Kila Kona, Kila Hatua Kasi Zaidi,” inaakisi juhudi za kampuni kuhakikisha huduma za mawasiliano ya 4G na 5G zinawafikia Watanzania kote nchini.

Amesema, “Kwa mwaka wa tatu mfululizo tumetambuliwa na kampuni ya kimataifa ya Ookla kama mtandao wenye kasi zaidi nchini Tanzania.

“Tunaendelea kuwekeza katika miundombinu ili kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na mawasiliano ya uhakika -iwe ni biashara, elimu, kilimo au kusherehekea mafanikio ya ushindi wa mbio kama hizi za Yas Kili International Half Marathon mtandaoni.”

Katika upande wa mazingira, Bacara amesisitiza dhamira ya Yas kuendeleza mradi wa Yas Green for Kili, unaolenga kulinda na kurejesha uoto wa asili kuzunguka Mlima Kilimanjaro tangu 2021.

“Mwaka huu tunapanda zaidi ya miti 50,000, na jana pekee tuliotesha miche 3,000 katika eneo la Njoro.

*Huu ni mchango wetu katika kuhakikisha Kilimanjaro inabaki kuwa alama ya fahari ya taifa letu,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, aliipongeza Yas kwa kuendeleza urafiki wa muda mrefu na jamii ya mkoa huo na kusema mbio hizo zimekuwa kichocheo cha utalii, biashara na maendeleo ya jamii.

Katika mbio za Yas Kili Half Marathon kwa mwaka huu, maelfu ya Watanzania walijitokeza kushiriki huku viwango vya ushindani vikipanda, na ushindi katika makundi mbalimbali ukitawaliwa na wanariadha wa ndani, jambo lililoleta hamasa kubwa miongoni mwa mashabiki.

Washindi wa jumla wa Yas Kili International Half Marathon (km 21)  ni pamoja na:-

Wanaume
Michael Geay – (TZ) muda;- 1:04:10
Josephat Joshua Gisumo (TZ) muda 1:04:14
James Kairiuki (KE) muda 1:04:30
Sule Elisante (TZ)
Benard Kiplagat (KE)
Dickson Paul (TZ)
Robert Makenzi(TZ)
Joshua Amos(TZ)
Boniphace Mwangi (KE)

Wanawake
Hamida Musa (TZ)
Failuna Matanga (TZ)
Veronika Wanjiku (KE)
Florence Wachira (KE)
Irene Mkungu (TZ)
Tunu Andrew (TZ)
Leah Bek (Germany)
Leah abeid (Germany)
⁠Everlyne Roytich (UG
Anisa badalo (TZ).