September 15, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasusi watakiwa kutumia programu ya “Darling Hair” kujiimarisha

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Dar

WASUSI mbalimbali hapa nchini wamehimizwa kutumia programu maalumu ya kampuni ya Darling Hair inayojulikana kama ‘Loyalty’ kujiendeleza kutokana na zawadi wanazoshinda.

Hayo yamesemwa katika hafla ya kusherekea miaka miwili ya programu ya Loyalty katika ukumbi wa Sinza Deluxe ambapo wasusi mbalimbali kutoka maeneo ya Tabata,Mbezi, Kimara na maeneo ya jirani walijumuika na kufanya shughuli mbalimbali kama mziki, michezo, kula pamoja na kujishindia zawadi mbalimbali.

“Programu hii sasa ina miaka miwili na tayari tumeona makubwa ambayo imetufanyia kama wasusi kwani baadhi yetu tumeongeza mitaji na wengine ambao walianza kama wasusi wa kuajiriwa sasa wana saluni zao baada ya kujishindia vifaa mbalimbali vya saluni,” amesema Salma Hamadi kutoka Tabata.

Pia ameipongeza kampuni ya Darling kwa kuwajali wasusi hapa nchini na kuwakutanisha kila mwaka kwa nia ya kuwapongeza na kuwazawadia kwa kazi nzuri.

Kwa upande wake Doreen Didas wa Mbezi Mwisho amewataka wasusi kuendelea kukusanya lebo kwa wingi ili wajiwekee nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi na kubwa kwa nia ya kutanua biashara zao zaidi.

“Unaweza kuwa msusi mdogo tu lakini Darling Hair wakakusaidia kukua pole pole kupitia program hii ya loyalty,”amesema Didas.

Shantel Mushi msusi kutoka Tabata Mawenzi amesema, “Natamani wasusi wote waijue program hii ya Loyalty kwani Darling wamekuja na kitu cha kipekee chenye faida kubwa mno kwa wateja yaani sisi wasusi,”.

Naye Angel Ngita msusi kutoka Tabata ametoa wito kwa wasusi kuwa wavumilivu na kulenga kupata zawadi kubwa ambazo zitawaongezea mitaji. “Mimi leo nimeshinda lakini sichukui zawadi hii,naendelea kukusanya pointi ziwe nyingi ili nipate kitu kikubwa zaidi, nimeingia kwenye program hii na malengo ili niweze kujiendeleza,”amesema.

Christina Mbando wa kutoka Tabata amesema“Hakuna kampuni inafanya kama Darling Hair tunawaomba wasiachie programu hii ili wasusi tuendelee kunufaika zaidi.”

Mwakilishi wa Darling Hair, Daniel Kisusange amesema,kampeni hiyo ya Loyalty inatarajia kuhamia mikoani ili wasusi wa mikoa mbalimbali nao wafikiwe.

“Tunawaomba mjiandae tunakuja huko maana kampeni hii ni ya nchi nzima na lengo ni kuendelea kuwafikia wasusi wengi zaidi,”amesema.Kisusange.

Alifafanua kuwa walianza na wasusi 5000 katika mwaka wa kwanza lakini sasa hivi wameshasajili zaidi ya 10,000 ambao wananufaika na program hiyo ya loyalty inayolenga kuwanyanyua wasusi wadogo ili wapate mitaji ya kujiajiri wenyewe.

Hata hivyo ametoa wito kwa wasusi waendelee kutumia program hiyo kujitanua zaidi kwani ni mpango wa kudumu wa kampuni hiyo.