
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wameitaka halmashauri hiyo kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha mianya yote inayosababisha upotevu wa mapato inazibwa.
Madiwani hao wametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichohusu uwasilishaji wa taarifa za makusanyo ya mapato katika kata.

Wamesema licha ya Halmashauri ya Nkasi kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, bado kuna umuhimu wa kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji na kudhibiti mianya yote inayoweza kusababisha mapato kupotea, ili fedha hizo ziweze kutumika katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Vicent Magendera, amesema halmashauri imepokea na kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na madiwani kuhusu namna ya kuongeza mapato sanjari nakuahidi kushirikiana Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha vyanzo vyote vya mapato vinakusanywa na mianya ya upotevu inazibwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Richard Masai, amewataka madiwani kuendelea kutoa ushirikiano kwa watendaji katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, akisisitiza kuwa mapato yanayokusanywa kwa ufanisi yataisaidia halmashauri kuimarisha utoaji wa huduma na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

More Stories
Kairuki: TTCL yafunguka, Tanzania yaingia kwenye Mapinduzi ya Kidijitali
OMDTZ yawezesha wananchi mipango kukabili mafuriko
Mradi wa Mawasiliano waongeza ufanisi huduma za Serikali