April 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanne washikiliwa kwa wizi wa injini

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Bukoba

Jeshi la polisi Mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa ( 04 ) kwa kosa la kupatikana na Injini ( 03 )za boti zinazodhaniwa kuwa za wizi.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Kagera Maketi Msangi,alithibitisha Hilo wakati akiongea na waandishi wa habari Mkoani humo.

Kamanda msangi,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussein Abdallah miaka ( 46)mkazi wa Nyamukazi Bukoba,Mwamed Juma miaka (24)mkazi wa Kashai Manispaa ya Bukoba,Richard Makwaya miaka (20) mkazi wa Kemondo na Japhet Pastory miaka (19 ) mkazi wa Geita.

Alisema watuhumiwa hao wote ni wavuvi na walikamatwa na Injini tatu za boti ambazo ni (Yamaha horse power 15 serial namba 1244882),(Yamaha horse poewa 15 serial namba 1315150 ) na ( Waterman horse power 99 serial namba R10007612.

Alisema pia walikamatwa wakiwa na mtumbwi wa mbao wenye namba BBKM 1296.

Alisema Injini hizo zinakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi Milioni ( 15.5)walipata taarifa za Siri kuwa Kuna watu wanatafuta wateja wa kuwauzia huku wakitaja Bei ndogo ukilinganisha na thamani halisi ya Injini hizo.

Alisema kufuatia taarifa hizo waliweka mtego na kuwakamata katika kisiwa Cha musira kata ya miembeni Manispaa ya Bukoba walifanikiwa kuwakamata wakiwa katika harakati za kusafirisha Injini hizo kuelekea Kisiwa Cha Goziba kilichopo Wilayani Muleba.

Alisema baada ya mahojiano watuhumiwa hao walishindwa kuthibitisha uhalali wa umiliki wa Mali hizo na kukiri kwamba walizipata kwa njia ya unyang’anyi wa kutumia silaha nguvu na vitisho dhidi ya Wavuvi ndani ya ziwa Victoria na Mara baada ya kuwanyang’anya huwatelekeza wavuvi ziwani.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Mara baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Kagera ACP Maketi Msangi akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani Injini za boti walizokamata zikiwa na watuhumiwa