April 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bima ya Afya (NHIF) kunufaisha watu wenye changamoto ya viungo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Serikali kupitia wizara Afya imejipanga kuhakisha wanaweka utaratibu wa huduma za watu wenye changamoto ya Viungo saidizi kuingizwa katika mfumo wa Bima ya Afya (NHIF)

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Tiba kwa Hospital zote hapa nchini luteni kanali Dkt. Pius Horumpende Wakati wa Mkutano ulio Wakutanisha wadau mbalimbali wanaojishugulisha na wauzaji na utengenezaji wa Vifaa Tiba saidizi wa watu wenye Ulemavu wa Viungo.

“Lengo la Serikali ni kuhakisha kuwa wananchi wanapata huduma hii muhimu kwa unafuu hasa kwa watu wenye uhitaji wa adha hiyo ya Vifaa Tiba saidizi vya Viungo vya watu hao”

Aidha ameaema Serikali itaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kutoa nafuu kwa vifaa muhimu kama hivyo vya vifaa tiba Viungo Ili kuhakisha wananchi wanapata huduma njema na wananchi kufurahia huduma za hospital zinazo tolewa hapa nchini.

Naye Rais wa chama Cha Watu wanao toa huduma ya Vifa Tiba na Viungo Saidizi ,Leah Baiki amesema kuwa mkutano huo una lengo la kuhakisha wanapeana uzoefu na kutoa elimu kwa Jamii juu ya huduma hizo wanazo zitoa.

Aidha Baiki ameongeza kuwa mkutano huo umeenda na maonesho ya kuonyesha shughuri zao wanazo zitoa kwa wananchi Ili waweze kufahamu huduma hizo sambamba na kufamiana kama wadau wa sekta hiyo muhimu katika nchi.