April 25, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanaume Summit 2026 kukutanisha washiriki zaidi ya  2,000

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza 

Zaidi ya wanaume 2,000 mkoani Mwanza,wanatarajia kushiriki katika kongamano la wanaume(wanaume summit 2026), lenye lengo la kuibua mjadala mpana kuhusu nafasi, changamoto na mustakabali wa mwanaume katika jamii ya kisasa.

Kongamano  hilo ambalo linafanyika kwa takribani mara ya 56, limeandaliwa na taasisi ya Wanaume Tanzania (Men at Work Global) pia katika tukio hilo taasisi hiyo itakuwa inaadhimisha miaka 11 ya gu kuanzishwa kwake(2015-2026).

Akizungumza Aprili 25,2026 na Waandishi wa Habari mkoani Mwanza,Rais na Mwanzilishi  taasisi ya Men at Work Global,Maxwell Shing’oma,amesema kongamano  hilo litafanyika Aprili 2026, jijini Mwanza.

Ambapo anaamini kupitia kongamano hilo sauti ya mwanaume itasikika kwa upana zaidi na kuchochea mabadiliko chanya katika jamii.

Maxwell  amesema, kongamano hilo litawakutanisha wanaume kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.Pia aliwakaribisha wanawake kushiriki ili kujenga uelewa wa pamoja na mshikamano katika familia na jamii kwa ujumla.

Pia amesema,katika kipindi  chote, taasisi hiyo imefanikiwa kuwafikia maelfu ya watu kupitia semina, makongamano na programu mbalimbali zilizofanyika maeneo ya shuleni, taasisi na vyuo vikuu.

Sanjari na hayo  amesema,taasisi hiyo  imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya malezi, uongozi na maendeleo binafsi kwa vijana na watu wazima, ikiwa na lengo la kujenga jamii yenye wanaume wanaojitambua na kuwajibika.

“Katika kongamano hili kutakuwa na mada mbalimbali  ikiwemo  afya ya akili,ambazo zitatolewa na  Joram Nkumbi,Timoth Kyara,Sam Salali,Shemeji  Melayeki na Charles Ndutu,litafanyika ukumbi wa chuoa cha Benki Kuu Tanzania(BOT),”amesema Maxwell.