April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wachezaji Polisi Tanzania waanza kuruhusiwa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BAADHI ya wachezaji wa kikosi cha Polisi Tanzania kilichopata ajali leo asubuhi walipokuwa wakitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC kurudi kambini wameanza kuruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC.

Katika ajali hiyo wachezaji 16, dereva pamoja na kiongozi walijeruhiwa huku mshambuliaji Gerard Mdamu akivunjika miguu yote miwili na dereva George Mketo akivunjia mbavu.

Wengine waliokuwepo kwenye gari hilo ni Abdullazizi Mkame, Pius Buswita, Daruweshi Saliboko, Deusdedity Cosmas, Salum Ally, Abdulmaliq Adam, Idd Mobby, Marcel Kaheza, Shabani Stambuli, Yahaya Mbegu, Datusi Pete, Mohammed Bakari, Mohammed Yusuph, Kassim Haruna na Christopher John.

Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni gari kuhama upande na kulikuwa na shimo hivyo dereva alipojaribu kulikwepa gari liligonga mti.

Mmoja wa wachezaji waliokuwepo kwenye gari, ameuambia mtandao huu kuwa, gari yao haikuwa kwenye mwendokasi kwani mwendo ulikuwa 40 na walishtuka kuona gari inahama njia na mbele kulikuwa na shimo.

Amesema, wakati dereva anajaribu kulikwepa shimo hilo aliuvaa mti na kwakuwa Mdamu alikuwa amesimama mlangoni alipata majeraha na kuvunjika miguu yote miwili.

RPC wa Kilimanjaro, Saimon Maigwa amesema, kutokana na ajali hiyo mchezo wao ujao dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Julai 14 ni ngumu kuchezwa kwani asilimia kubwa ya wachezaji wao tegemeo ndio waliopata ajali hivyo kama viongozi watakaa na kuandika barua kwenda Bodi ya Ligi (TPLB) kuona kama utaweza kusogezwa mbele.

“Kama viongozi tumeumizwa sana kwani mategemeo yetu yalikuwa kushinda mechi zetu zilizosalia hivyo uongozi utakaa haraka sana ili kuona kama mechi zetu zinaweza kusogezwa mbele. Lakini pia tunaushukuru sana uongozi wa KCMC kwa huduma walizowapatia wachezaji wetu