May 9, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uvuvi haramu kilio cha umaskini wavuvi Ziwa Victoria

Na Penina Malundo, timesmajira

MWENYEKITI wa Umoja wa Wadau wa Uvuvi Mkoa wa Mara na Ukanda wa Ukerewe Ziwa Victoria,Matete Mgongo amesema kukithiri kwa uvuvi haramu katika ziwa victoria umesababisha hali ya umaskini kwa wavuvi wengi hali inayopelekea kushindwa kumudu maisha yao.

Akizungumza jana kwa njia ya simu Mwenyekiti huyo,Mgongo alisema hawajui hatima ya maisha yao kwani wanategemea uvuvi katika kuendesha maisha yao ila kwa hali ya sasa uvuvi haramu umeweza kukithiri kwa kiwango kikubwa tofauti na nchi ya Uganda na Kenya.

Amesema kwa Mkoa wa Mara pekee watu wanaofanya shughuli za uvuvi na wale wanaotegemea shughul hizo takwimu zinaonyesha uvuvi zaidi ya laki 5 wanategemea uvuvi kwa mkoa wa mara.”Tunapozungumza kero ya uvuvi haramu imetuwekea katika mazingira tata kwani mkoani kwetu kulikuwa na kiwanda kimoja cha kuchakata samaki cha Musoma Fish lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili sasa kiwanda hicho hakifanyi kazi,”alisema na kuongeza

”Viwanda kama Musoma Fish vinafungwa ni kutokana na samaki kutokuwepo kwa wingi na hii imetufanya kuwa na masikitiko makubwa kutokana na uvuvi huu haramu kusababisha hali ya umaskini katikatika yetu,”amesema.

Amesema hali ya uvuvi haramu unavyokithiri nchini tumekosa imani na walinzi wa mali zetu,maafisa uvuvi,wafawidhi wote wameajiliwa na serikali lakini ukiuliza hatusubutu wao hata kuzungumza kama wazalendo.

“Vita tunavyopigana sisi tunaamini ziwa ni titi la mama kila mtu ananyonya ziwa hili kwani sisi tumerithishwa na sisi tunatakiwa kurithishiana kwa kufanya uvuvi kulinda samaki kisheria,”amesema.

Kwa upande wake Mvuvi wa mwalo wa Iriga musoma mkoani mara, Nyanja Meli,amesema uvuvi haramu ni uvuvi ambao umekuwa unawaathiri kwa kiasi kikubwa wao kurtokana na uvuvi huo kuvua sagara katika mazalia yake bila muda wao kufika wa kuvuliwa.

Amesema wavuvi wa nchi jirani Kenya na Uganda ambao nao wanatumia ziwa hilo wamekuwa wanalinda rasilimali zao kwa hali ya juu kutokana na kujua faida wanayopata katika ziwa hilo kwao na vizazi vyao.

”Serikali ingeteua kikosi kazi maalum cha JKT ambao wangekuwa na maboti maalum ambayo lingekuwa linafanya patrol katika kila kisiwa kuhakikisha hali hii ya uvuvi haramu inakomeshwa na wahusika kuchukuliwa hatua stahiki,”amesema.