May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahasibu, wakaguzi zingatieni maadili – Simbachawene

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Boniface Simbachawene amewasisitiza wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania kuendelea kutimiza malengo kwa kuzingatia maadili, nidhamu na uaminifu katika kufanya kazi na kukuza taaluma nchini.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa mwaka wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA) uliofanyika jijini dar es salaam ambapo wahasibu na wakaguzi zaidi ya 2000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wamekutana kujadili mambo mbalimbali yanayohusu fani hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na mkaguzi wa hesabu Tanzania NBAA Prof. Sylivia Temu amesema kufanya vibaya kwa wanafunzi kwenye somo la hesabu wanaohitimu kidato cha nne kunasababisha kudhohofisha fani hiyo kwa kukosekana kwa wahasibu wapya.

“kukua kwa fani hiyo kunategemea zaidi wanafunzi wanaohitimu hivyo kutofanya vizuri kwenye somo la hesabu kunazidi kudhorotesha fani hiyo ni vyema serikali kupitia wizara ya elimu kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo” Prof. Sylivia Temu

hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius Maneno amesema matumizi ya Tehama yanatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa wahasibu nchini ili kuendana na kasi ya utendaji kidigitali.