March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uingereza yapigwa faini Euro 30,000

LONDON, England

CHAMA cha Soka England, kimetozwa faini ya Euro 30,000

baada ya mashabiki wake kummulika usoni kipa wa

Denmark,Kasper Schmeichel kwa tochi yenye mwanga mkali

wakati wa mechi ya nusu fainali michuano ya Euro 2020 ,

mchezo uliofanyika Jumatano kwenye Uwanja wa Wembley.

FA, walishtakiwa Alhamisi kwa matumizi ya tochi yenye

mwanga na wafuasi wake,kutokana na kumsababishia

usumbufu kipa huyo na kuchangia Denmark kukubali

kichapo cha goli 2-1.

Shabiki alielekeza laser machoni mwa Schmeichel wakati

Nahodha wa England Harry Kane alijitokeza kuchukua

adhabu ya kutatanisha katika muda wa nyongeza,

iliyotolewa baada ya

winga Raheem Sterling kuangushwa

na kiungo

Mathias Jensen.

Mashabiki katika uwanja huo pia walisikika wakizomea

Wimbo wa Taifa wa Italia kabla ya kuanza.

Chama Cha Soka

Ulaya (UEFA) kilisema katika taarifa yake leo “UEFA

imeamua kuipiga faini Chama cha Soka cha England euro

30,000 kwa matumizi ya tochi na kusababisha usumbufu

wakati wa nyimbo za taifa na kuweka fataki.

Zaidi ya mashabiki 60,000 watakubaliwa huko Wembley

kwa

fainali siku ya Jumapili wakati England wanatafuta

kushinda katika mashindano makubwa tangu Kombe la Dunia

la 1966.