May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ufaransa yaleta mabilioni nchini, uwekezaji mkubwa waja

Na David John,TimesMajira Online

SERIKALI ya Ufaransa kupitia ubalozi wake nchini Tanzania Imesema kuwa dola bilioni 4. 2 kupitia makubaliano ya sekta za umma na binafsi za ufaransa inatarajia kuwekezwa hapa nchini.

AKizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar Es Salaam kwenye ofisi za ubalozi wa ufaransa nchini Tanzania ambao pia uliohudhuriwa na baadhi ya wawekezaji wa ufaransa hapa nchini.

Nabil Hajlaoui amesema uwekezaji huo mkubwa unatokana na Ziara ya Rais Samia Hassan Suluhu nchini ufaransa.

Hajlaoui amesema Kuwa Makampuni 40 Kutoka ufaransa ( B pfrance, Business France na MEDEF International ) wataalamu kutoka sekta mbalimbali – Usafiri, Nisharti,Maji safi,Kilimo-Chakula na afya. Zinalenga dhamira ya kuja nchini ili kukidhi mfumo wa Ikolojia wa Tanzania umma / binafsi kwa lengo la kukidhi mahiji ya soko.

“Ndugu waandishi ujumbe huu makubwa unatokana na matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Ufaransa aliyoifanya Februali. 2022 na Ziara ya Waziri wa ufaransa anayeshughulikia Biashara Nje na Vivutio vya Uchumi, Franck Riester jijini Dar es Salaam Mwezi OKtobar 2021.”amesema Hajlaoui

Amesema pia Ziara hiyo imechochewa na nia ya dhati ya Makampuni ya Ufaransa kwa Tanzania na hii nikutokana na ukuaji wake na utulivu wa kisiasa ,inatoa matarajio makubwa ya maendeleo kwa wataalamu wa ufaransa .

“Fursa hizi zinatia matumaini zaidi Kwani nchi inajitahidi kurejesha hali ya biashara inayowafaa wawekezaji wa kigeni. Wakati wa mkutano wake na jumuiya ya wafanyabiashara wa ufaransa mjini Paris Mwezi wa pili 14 mwaka huu nchini ufaransa Rais Samia alisisitiza juu ya mageuzi yake ya “biashara bora” na akatumia fursa hii kukaribisha Makampuni ya Ufaransa kuja Tanzania. Amesema

Ameongeza kuwa Miezi tatu baada ya mwito huo makampuni kutoka nchini ufaransa yaliitikia, na Makampuni haya ufaransa yaliitikia kwa wingi wito huu na kupata heshima kubwa ya kukutana na Rais jijini Dar Es Salaam kumjulisha maendeleo ya miradi yap.

Hajlaoui amesema ufaransa ambapo kwa sasa inashikilia wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya ,pia inakusudia kuisadia Tanzania kuhamasisha vyombo vya ushirikiano wa ulaya. Ikiwamo mpango wa Global Gateway ( hadi Euro bilioni 300 katika uwekezaji) Ili kuipa nchi miundombinu bora na endelevu.

Amesema Kuwa idadi ya Makampuni ya Ufaransa nchini Tanzania imeongezeka zaidi ya mara tatu kuazia mwaka 2019 hadi 2022(Makampuni40 mwaka 22022 ikilinganishwa na12 mwaka 2,019 )hivyo uwepo wa ufaransa umepanuka na kuongezeka kwa idadi ya biashara ndogo na Kati na za ukubwa wa Kati na zinazoungwa mkono na ofisi za kikanda ya biashara ya ufaransa.

Hajlaoui amefafanua Kuwa Makampuni ya nakusanyika nchini Tanzania pamoja na washirika wa Tanzania katika mkakati wa muda mrefu na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi.” wamethibitisha kuendelea kudumisha uhusiano kupitia miradi na uwekezaji wao nchini licha ya changamoto inayohusishwa na janga la Covid-19.

Pia amesema ufaransa iko mbioni Kuwa mwekezaji mkuu wa Ulaya nchini Tanzania, kwa sababu ina nia ya kuongeza ushiriki wake wa moja kwa moja katika miradi ya maendeleo ya nchi hasa usambazaji na uzalishaji wa nishati, kupitia makampuni ya ufaransa Kama vile Engie, total Energies na Maurel na prom, Usafiri na vifaa, ushirikiano na Airbus na mradi wa ukarabati wa terminal ya pili katika uwania wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Pia amesema miradi mingine ni Boutiques Batiment baharini (mradi wa bandari ya bagamoyo ) maji na Usafi wa mazingira ,mawasiliana ya simu ( yaliyozinduliwa hivi karibuni na Eutelsat ya huduma yake ya mtandao ya kasi ya satelaite kupitia kampuni tanzu ya konnect Broadband Tanzania) na afya ( mradi wa hospitali ) Dodoma ,Msaada kwenye vituo vya saratani nchini Kote.