May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tukusanye taarifa za kijografia kwa kila nyumba tunayoitambua

Na mwandishi wetu, Timesmajira online

Naibu katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amekemea tabia ya wachukua taarifa wasio waadilifu wanaochukua taarifa za kijiografia (GPS) za sehemu moja kutolea taarifa kwenye eneo jingine. Jambo hilo linaharibu kazi data na linasababisha mfumo kutoa taarifa zisizosahihi.

“Watendaji mkagaue na kujiridhisha kuhusu taarifa za kijiografia (GPS), hasa pale inapotokea taarifa hizo kufanana eneo moja na jingine allisema Naibu Katibu Mkuu Mmuya.”

Hayo yamesemwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa operesheni ya anwani za makazi katika wilaya ya Kilwa na Rufiji. lazima tukusanye taarifa za kijiografia kwa kila nyumba ambayo inaenda kutambuliwa kwa sababu taarifa hizo za kijografia zinatofautiana.

“Ninawapongeza wananchi wa Kilwa na Rufiji kwa uelewa na muitikio wao katika kutekeleza Operesheni ya anwani za makazi, na umuhimu wake kwa Sensa ya watu na makazi. Tuendelee kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa operesheni ya anwani za makazi.”

“Ninatoa wito kwa wananchi wote, kujiwekea namba ya kudumu kwenye mageti au milango ni jukumu lao alisema Naibu Katibu Mkuu Mmuya.”

Akihitimisha Injinia wa Tarura Agatha Mtwangambate amesema kwa awamu ya kwanza idadi ya vibao vya barabara ni kwa ajili ya barabara zote zilizosajiliwa, na vitawekwa katika mwanzo wa barabara na mwisho wa barabara. Kadri operesheni ya anuani za makazi inavyoendelea tutaanza kuzitambua barabara mpya na kuziwekea vibao.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza na wananchi katika barabara ya Matumbi kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akimsikiliza Mwananchi katika Mtaa wa Mkwanyule akijieleza jinsi alivyopokea operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rufiji Mhe. Juma Ligomba Na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rufiji Bwn. John Kayombo mbele ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Rufiji wakati akikagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya (katikati) akitembea katika Mtaa wa Mkwanyule kukagua utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza jambo na Mtendaji wa Kijiji cha Umwe Kaskazini kata ya Umwe Bwn. Emmanuel John katika kukagua utekelezaji Operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Rufiji.