Na Zena Mohamed,TimesmajiraOline,Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA),Prof.Joseph Ndunguru amesema Takwimu za mwaka 2024/25 zinaonesha kunautoshelevu wa chakula kutoka asilimia 128 hadi 130 ambapo inaweza kuzalisha mazao ya chakula takribani Tani Mil.23.
Prof.Ndunguru amesema hayo jijini hapa leo Machi 24,2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli za Mamlaka hiyo ambapo amesema katika asilimia hizo TPHPA inamchango mkubwa kwasababu wao ndiyo wanadhibiti visumbufu ambavyo vingeweza kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.

Amesema Tanzania kuliwahi kutokea mlipuko wa baa la panya katika mikoa 16 muhimu ya Kilimo,Wilaya 68,Kata 638 na Vijiji 1669 na Mamlaka hiyo ilikwenda kudhibiti panya hao kwa wakulima zaidi ya 66,511 na kuweza kuokoa Ekari 400,008 za mazao ya wakulima hao.
Aidha amezungumzia jinsi walivyodhibiti ndege aina ya kweleakwelea ambapo amesema kulikuwa na uvamizi wa ndege hao hasa kwenye skimu kubwa za mazao ya nafaka ya mpunga.
“Kweleakwelea Mil.231 walivamia maeneo ya Mbarali,Kapunga,Mbeya,Ruvu,Simiyu na maeneo mengine katika Halmashauri 23,kwahiyo tulienda tukafanya udhibiti wa ndege wale na tukaweza kuokoa tani za mazao 1,600,000 ikiwemo Mpunga,Uwele na Mtama.
“Udhibiti huu unafanyika kwa kutumia ndege maalum ya kisasa na ndege Nyuki(Drones)pamoja na vinyunyizi vya mbereko ambavyo vinafanywa ardhini,”amesema.
Vilevile alizungumzia udhibiti wa Viwavijeshi ambapo amesema ni wadudu waharibifu wa mazao na wanaathiri mazao mengi ikiwemo Mahindi ambapo TPHPA imeweza kudhibiti viatarishi kwenye Ekari za Mazao 219411 katika Wilaya 49 kwahiyo kufanya udhibiti huo waliweza kuokoa tani za mazao 529347.


More Stories
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni.
Kero za Walimu kutoshughulikiwa kwa wakati chanzo Cha msongo wa mawazo-CWT