TMA yaeleza faida taarifa hali ya hewa
Na Joyce Kasiki, Dodoma
Afisa Masoko wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Nasry Msulwa, amesema matumizi ya taarifa za hali ya hewa yameendelea kuwa nyenzo muhimu katika kusaidia wananchi na wadau mbalimbali kufanya maamuzi sahihi na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na matukio ya hali mbaya ya hewa.
Msulwa ametoa kauli hiyo leo Juni 23 ,2026 katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, ambapo TMA inatoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za hali ya hewa na namna zinavyoweza kutumika katika shughuli za kila siku.
Amesema mamlaka hiyo imejikita katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za hali ya hewa kwa wakati, zikiwemo utabiri wa kila siku, utabiri wa msimu na tahadhari za matukio hatarishi, ili kuwawezesha kupanga shughuli zao kwa ufanisi zaidi.
Kwa mujibu wa Msulwa, sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, usafiri wa anga, usafiri wa majini pamoja na usimamizi wa maafa ni miongoni mwa sekta zinazotegemea taarifa za hali ya hewa katika kupanga na kutekeleza shughuli zake.
Aidha, amesema TMA imekuwa ikitumia maonesho hayo kuonesha teknolojia na mifumo inayotumika katika ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa, hatua inayowasaidia wananchi kuelewa mchakato wa utoaji wa utabiri na tahadhari mbalimbali.
ya wananchi waliotembelea banda la TMA wameeleza kufurahishwa na elimu wanayopewa, wakisema taarifa za hali ya hewa zimekuwa msaada mkubwa katika kupanga shughuli zao za kiuchumi na kijamii pamoja na kujikinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi

More Stories
Wananchi wapata elimu ubora,usalama na bidhaa
Mkomi Aridhishwa na Utendaji wa PSSSF
Matumizi magari ya umeme kuongeza umuhimu gesi asilia