Na Judith Ferdinand, Mwanza
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza,imefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 16.6, kwa mwaka wa fedha 2025/2026 sawa na asilimia 101 ya mapato ya ndani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ummy Wayayu,Agosti 5,2026 akitoa taarifa katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo,kwa kipindi cha mwaka mzima wa fedha 2025/2026(Julai-Juni),ambapo amesema hadi kufikia Juni 30,2026,halmashauri hiyo ilikuwa imevuka lengo kwani kwa mwaka huo wa fedha iliidhinishiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya sh.bilioni 16.4 katika bajeti ya mapato ya ndani.

Wayayu amesema,katika kipindi cha Julai 2025 hadi Juni 2026,halmashauri hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali yenye kiasi cha zaidi ya sh.bilioni 47.3,kati ya kiasi
hicho zaidi ya sh.bilioni 4.2,ni fedha za mapato ya ndani na zaidi ya sh.bilioni 43.1,kutoka Serikali Kuu.
Amesema utekelezaji wa miradi hiyo umegawanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo utawala zaidi ya sh.bilioni 4.2,sekta ya afya zaidi ya sh.bilioni 1.5,sekta ya elimu msingi zaidi ya sh.bilioni 2.4,sekta ya elimu sekondari zaidi ya sh.milioni 935 na sekta ya miundombinu(TACTIC) zaidi ya sh.bilioni 38.2.
Sanjari na hayo Wayayu amesema,Mei 12,2026 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Said Mtanda alifanya ziara katika halmashauri na kufanya mkutano
wa hadhara uliohusisha Kata za Sangabuye, Bugogwa na Kayenze.Katika mkutano huo ambapo aliagiza
wananchi walipwe fidia mara moja.
“Mpaka kiasi cha zaidi ya sh.bilioni 1.2, zimelipwa kati ya zaidi ya sh.bilioni 5 ambazo halmshauri inadaiwa,”amesema Wayayu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyasaka Fredy Kisaka,ametoa pongezi kwa kufanikisha kufikia zaidi ya lengo la makusanyo ya mapato ya ndani,hivyo alishauri jitihada zaidi ili kufikia malengo ya mwaka 2027.
Naye Diwani wa Kata ya Pasiansi Regina Lubala amesitiza,ushirikishwaji uendelee pamoja na mshikamano na upendo kwani kupitia vitu hivyo wameweza kuona matokeo.



More Stories
Watakiwa kuhamasisha vijana kuchapa kazi
Serikali yahakikisha vyakula vya samaki havileti madhara
Waziri Mbarawa ashuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya TRC