April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TBS yataka wakulima kuongeza thamani ya mazao

Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewahimiza wakulima kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha kwa kuhakikisha wanafungasha vizuri kwa kutumia vifungashio vilivyothibitishwa na shirika hilo.

Hayo yasemwa leo na Ofisa Uhusiano mkuu wa TBS, Roida Andusamile alipokuwa akizungiumza na Mtandao huu katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nane nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Andusamile amesema, maonesho ya wakulima ya mwaka huu wamejikita katika kutoa hamasa na elimu ya umuhimu wa kuongeza thamani ya mazao yao ambayo itawasaidia kuongeza fedha na kupata masoko kwa urahisi.

Amesema, ni muhimu kwa wakulima kuchakata mazao yao kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali pamoja na kutembelea Shirika hilo ili kupata ushauri wa kitaalam juu ya namna ya kupata vifungashio vyenye ubora sambamba na kuzingatia uzalishaji wenye tija.

Kupitia maonesho hayo, TBS wameahidi kukutana na watu wengi ambao ni wazalishaji, watumiaji wa bidhaa mbalimbali hasa wakulima ambao wanazalisha na kupeleka sokoni tu ili kuongeza thamani ya mazao.

Hata hivyo amesema kuwa, baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza bidhaa ambazo ni hafifu sokoni na jambo ambalo limewafanya kujipanga kikalimifu kuhakikisha wanadhibiti Hali hiyo kwa kufungua ofisi katika mipaka yote.