Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki na kushinda tuzo ya Ubora katika Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Uchumi.
Tuzo hizo za sekta ya Umma zinaangazia ubunifu unaofanywa na taasisi mbalimbali za umma kwa muktadha wa kutoa huduma bora zinazoakisi maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania.
TanTrade imekua ikifanikisha hayo kupitia Maonesho ya Sabasaba, kuratibu Maonesho mbalimbali ya Kimataifa kama vile Expo’s, Mifumo mbalimbali ya Kidigitali ya Biashara kama vile Trade Portal, Biashara App.
Hafla ya tuzo hizo zimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

More Stories
UWT yahimizwa kusimamia malezi bora
Uwekezaji wa Michezo wavutia Watalii Tanzania
Mkurugenzi Bonde Rufiji, ahimiza utunzaji vyanzo vya maji