Na Mwandishi wetu,Timesmajiraonline
HUDUMA za afya ya mama na mtoto katika ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa zimeendelea kuimarika ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika ununuzi wa vifaa tiba na kutoa mafunzo kwa watoa huduma ikiwemo madaktari na wauguzi.
Kauli hiyo imetolewa leo Julai 22, 2026 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Prof. Palamagamba Kabudi wakati akizindua jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Vijimbweni Kigamboni Jijini Dar es salaam.

Amesema , Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alianza kusimamia jambo hili tangu akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndio maana Umoja wa Afrika ulimteua kuwa kinara wa afya ya mama na mtoto katika Bara la Afrika.
Aidha, Prof. Kabudi,amefafanua “Maendeleo haya katika kipindi cha Miaka 65 ya Uhuru ni hatua kubwa ukilinganisha na kipindi ambacho Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere anaichukua nchi kutoka kwa mkoloni, hali ilikuwa na tofauti na sasa, ni lazima tujivunie maendeleo tuliyofikia”.

Awali Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mikaya Tumaini Dalmia ameishukuru serikali kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya ya afya akisema awali wananchi wa Kigamboni walikuwa wanafuata huduma katika Hospitali ya wilaya ya Temeke na Mhimbili.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Haran Sanga ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwarahisishia wananchi wa kigamboni kupata huduma karibu na maeneo wanayoishi.



More Stories
Masoko ya machinga kufungua fursa kwa vijana nchini
Mwanasheria Mkuu afungua mkutano wa Mwaka wa TIArb
Kituo cha afya Ibungilo chafikia asilimia 25