April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Simiyu yafanya vema mashindano ya Tenisi

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

WACHEZAJI wa Tenisi kutoka timu ya Mkoa wa Simiyu wameendelea kufanya vema katika mashindanoya Tenisi ya BQ baada ya wachezaji wake wote wanne kuingia hatua ya nusu

Mashindano hayo yanayofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam yakishirikisha watoto zaidi ya 125 kutoka mikoa zaidi ya mitano ambao wameonesha vipaji vya hali ya juu.

Wachezaji wa Simiyu waliotinga nusu fainali ni Rebecca Kulwa, Rodha Joseph, Hellen Mtaka na Martha Mtaka.

Katika mechi zao walizocheza jana, Rebecca Kulwa (Simiyu) aliibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Nasma Jumanne wa Dar es Salaam huku Martha Mtaka wa Simiyu akambwaga Yusra Majaliwa wa Dar kwa seti 2-0.

Katika mchezo mwingine, mchezaji Hellen Mtaka aliib uka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Janemary Michael kabla hajambwaga Nyakwera ambaye pia ni wa Dar kwa seti 2-1.

Akizungumzia mafanikio ya timu yake, Kocha wa Simiyu, Mikidadi Bunaya amesema kuwa, kujituma kwa wachezaji wake kunatokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya wakipata sapoti kubwa ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.

Pia amewaomba wadau wengine wa michezo kutoka Mkoani humo kujitokeza na kuendelea kusapoti michezo mbalimbali ili kuibua kuendeleza na kuibua vipaji vya watoto.